Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, June 9, 2014

Msaada wa Matibabu kwa Mtoto Maimuna Yahaya (11 yrs old)

 

 Pichani ni Mtoto Maimuna Yahaya
 Mtoto Maimuna Yahaya akiwa na Mama yake Mzazi  Tunu Juma

Msaada wa Matibabu kwa mtoto Maimuna Yahaya Mtoto Maimuna Yahaya (11) anayesoma shule ya Msingi ya watoto wenye mahitaji maalum (wenye ulemavu) ya Irente Rainbow (Lushoto- Tanga) Darasa la pili, anasumbuliwa na tatizo la mifupa na ukubwa wa kichwa tangu kuzaliwa kwake, tatizo lililompelekea kuwa na ulemavu wa viungo na mtindio wa Ubongo.

Mama wa mtoto huyo, Bi. Tunu Juma Maziku amesema amekuwa akimpeleka mwanae huyo Maimuna katika hospitali ya KCMC kwa muda wa miaka 11. Hali ya mtoto inaendelea kuimarika, anaweza kukaa na anaweza kuongea.
Bi. Tunu amekuwa akimpeleka mwanae huyu shule na kumsubiri hadi wamalizapo masomo ya siku na kumrejesha nyumbani kwa muda wa miaka miwili. Bi. Tunu Juma Maziku  anasema kwa sasa hali yake ya kiuchumi si nzuri, anashindwa kumpeleka mwanae kuhudhuria matibabu KCMC, hivyo anaomba msaada wa kifedha kwa wasamalia wema ili mtoto wake aendelee na matibabu.   Mahali wanapopatikana: Lushoto Mabwawani  

Mawasiliano: Namba ya simu ya mama mzazi: +255712504768 Namba ya Tigo Pesa mesajiliwa kwa Jina la Maimuna Yahaya +255655779345 na Namba ya Airtel Money ni 0787204160 imesajiliwa kwa jina la Tunu Juma.

Chanzo: Vijimambo

No comments :

Post a Comment