Rais Dkt Jakaya Kikwete akiongea na viongozi wa Jumiya za Kitanzania zilizopo Toronto, Canada siku ya Ijumaa May 30, 2014. Rais Dkt Jakaya Kikwete alikuwa Canada wiki iliyopita kuhudhuria kikao cha “Improving the Lives of Women and Children: Maternal, Newborn and Child Health “. Viongozi wa ZANCANA walipata fulsa ya kumweleza Mheshimiwa Rais Jumuiya yao inavyojitahidi kusaidia nyumbani Tanzania katika sekta mbalimbali hususan ikijikita kwenye elimu na mahospitalini kwa kupeleka misaada mbalimbali mashuleni na kwenye Wizara ya Afya na ustawi wa jamii.
Viongozi wa Jumuiya mbalimbali za Watanzania Toronto, Canada wakimsikiliza Rais Dkt. Jakaya Kikwete alipokuwa akiongea nao siku ya Ijumaa May 30, 2014.
Kushoto mwisho (mwenye miwani) ni Shk Omar Ali Said ambae ni Rais wa Jumuiya ya ZACADIA (Zanzibar-Canadian Diaspora Association). Jumuiya ya Zacadia ikishirikiana na PBZ Ltd na World Remit ndio iliyoleta kwa Watanzania wanaoishi nje mfumo wa kisasa ambao ni wa haraka, rahisi na wakuaminika wa kupeleka pesa nyumbani kupitia internet. Kwa maelezo zaidi tembelea website ya PBZ Ltd. Pia, mwisho wa wiki hii au mwanzo wa wiki ijayo kutokana na shinikizo la Zacadia Watanzania kutoka Diaspora communities zote duniani wataweza kupeleka pesa nyumbani kupitia simu za mikononi za jamaa zao. Pesa zitaweza kufika sehemu yoyote ile nchini penye simu ya mkononi. Kuwepo kwa branch ya PBZ haitokuwa tena ni lazima ili mtu aweze kupokea pesa kutoka kwa jamaa yake anaeishi nje. Zacadia ni Jumuiya ya mwanzo katika Jumuiya za nje za Wazanzibari zinazojihusisha na Zanzibar Diaspora.
Makamu wa Rais wa ZANCANA Jamal Jiddawy katika picha yaa pamoja na Rais Dkt. Jakaya Kikwete.
Executive Manager Bishara na Board Member Zamil wa ZANCANA wakiwa kwenye picha ya pamoja na Rais Dkt Jakaya Kikwete.
Source: Vijimambo (edited by ZNK)
No comments :
Post a Comment