Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, August 26, 2014

ADC wapongeza uamuzi wa Hamad Rashid


Na Daria Erasto, Mwananchi
Dar es Salaam - Chama cha Aliance for Democratic Change (ADC), kimesema kimepokea kwa furaha kauli iliyotolewa na Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashidi Mohammed ya kutaka kugombea nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho na kusema kuwa ameonyesha ukomavu mkubwa wa kisiasa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa ADC Taifa, Said Miraaj Abdulla alisema chama chake kinamkaribisha yeye pamoja na Watanzania wote kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kupitia chama hicho.
Mwenyekiti huyo, alisema Hamad ameonyesha ukomavu kwani ameamua kuwatumikia wananchi kwa kuamua kujiunga na chama hicho alichodai kuwa ni kichanga kikilinganishwa na alichotoka cha CUF ambacho kina zaidi ya miaka 20 sasa tangu kianzishwe.
“Si jambo rahisi kwa mtu kuacha chama ambacho kina sifa ya kuwa wapinzani kwa zaidi ya miaka 20 na kutaka kujiunga na chama chenye umri wa miaka miwili tu, huu ni ujasiri wa aina yake, tunawakaribisha watu wote wenye mtazamo kama huo, waje tushirikiane kujenga demokrasia nchini,” alisema.
ADC pia imemtaka Katibu Mkuu CCM, Abdulrahman Kinana kuharakisha mchakato wa mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi suala la Ukawa kugomea kushirikia vikao vya Bunge Maalumu la Katiba.

No comments :

Post a Comment