Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, August 29, 2014

Mgawanyo wa fedha Bara, Zanzibar waibua mvutano

Mgawanyo wa fedha za Muungano kati ya Tanzania Bara na Zanzibar umekuwa moto mkali, baada ya kuendelea kuleta mvutano mkali katika suala hilo ambalo ni moja ya mambo yanayoutikisa muungano.

Hali hiyo ilijidhihirisha wazi kwa mara nyingine jana wakati wa semina maalum iliyoandaliwa na Bunge Maalum la Katiba kwa wajumbe wa Bunge hilo.

Semina hiyo ambayo watoa mada wakuu walikuwa, Gavana wa Benki Kuu ya Taanzania (BoT), Prof. Benno Ndulu, na makatibu wakuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile upande wa wa Tanzania Bara na Khamis Mussa, upande wa Zanzibar, iliitishwa ili kutoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Bunge hilo ambao wamekuwa katika sintofahamu kubwa juu ya suala hilo wakati wa mijadala kwenye kamati zao kiasi cha kutofikia mwafaka.

Ndulu na Makatibu wakuu hao waliitwa kutoa ufafanuzi huo baada ya kuibuka mvutano kwa wajumbe hao na kusababisha baadhi ya kamati kuacha kiporo cha Sura ya 14 ya rasimu ya Katiba baada ya kukosa mafikiano juu ya muundo wa benki kuu na uanzishwaji wa mfuko wa fedha wa pamoja.

Habari kutoka ndani ya semina hiyo zinasema kuliibuka mvutano mkali juu ya mgawanyo wa fedha hizo unavyopaswa kuwa baina ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania pamoja na wajumbe wa Tanzania Bara na Zanzibar

Chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya semina hiyo, kilieleza kuwa wakati upande wa Zanzibar ulitaka ziundwe Benki tatu ya Zanzibar, Tanzania Bara na Muungano, wajumbe wa Tanzania bara walipinga na kueleza kukubali muundo huo ni sawa na kurejea kwenye rasimu ya serikali tatu.

“Ndani kulikuwa na mvutano mkali, hata makatibu wa Fedha walionekana kutofautiana kimsimamo kuhusu namna ya muundo wa benki kuu,” kilisema chanzo hicho.

Hata hivyo, Gavana Ndulu, aliwaeleza wajumbe hao kwamba mfumo wa kuwa na Benki kuu tatu kwa mfumo wa serikali mbili ambao umependekezwa kwenye kamati badala ya mfumo wa serikali tatu ambao upo katika Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ni kitu ambacho hakiwezekani.

“Profesa Ndulu, alituambia ubaya wa muundo uliopendekezwa na rasimu kuwa na Benki kuu kwa kila nchi washirika, alisisitiza mfumo wa sasa unakidhi mahitaji,” kilisema.

Akitoa maoni yake binafsi kuhusu semina hiyo, Mjumbe wa Bunge hilo, Hamis Dambaya, alisema kutofautiana kulitokana na baadhi ya watu kutokuwa na uelewa wa mambo ya kiuchumi na lugha za kitaalamu kuhusu fedha.

“Wataalamu wametueleza ubaya wa muundo wa Benki kuu kuwa tatu, walituambia kwa nini serikali ya Muungano inakopa na ile ya Zanzibar haina fursa hiyo, wote tumeelewa tunasubiri kurudi kwenye kamati zetu kutatua suala hili,” alisema Dambaya.

Aidha, Dambaya, alisema ufafanuzi huo uligusa katika suala la mgawanyo wa mapato, ambapo wamegundua inakwenda vizuri tofauti na maneno yanayotolewa nje ya Bunge hilo.

Chanzo hicho, pia kilisema Katiba Mkuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar, Mussa, alionekana kutofautiana na Profesa Ndulu kuhusiana na suala la kuwa na benki tatu.

CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment