Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, September 14, 2014

BAWACHA

Halima Mdee ndiye Mwenyekiti Mpya BAWACHA

Mwenyekiti mpya wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA, Halima Mdee akizungumza baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa baraza hilo. (picha: Francis Dande)

Mbunge wa jimbo la Kawe Mheshimiwa Halima James Mdee, ameshinda kiti cha Uenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) baada ya kupata kura 165 huku mtu aliyemfuatia kwa karibu akipata kura 35. Akiongea na ITV mara baada ya kupata matokeo hayo, mbunge huyo amesema matokeo hayo yamedhihirisha ni kwa jinsi gani anakubalika kwa wakinamama ndani ya chama hicho.


Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA Taifa (BAWACHA), wakifungua shampeni kusherehekea ushindi wa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA Taifa, Halima Mdee (kushoto) baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo.

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (Bara), Hawa Mwaifunga akilia kwa furaha baada ya kushinda nafasi hiyo katika uchaguzi uliofanyika juzi.


Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA wakiwa katika mkutano huo.


Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA Taifa, Halima Mdee (kulia) akipongezwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa Baraza la Wanawake wa Chadema. Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (Bara), Hawa Mwaifunga.


Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA Taifa, Halima Mdee (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wake (Bara), Hawa Mwaifunga (kushoto) na Makamu Mwenyekiti (Zanzibar), Hamida Abdallah.

Halima Mdee

cHANZO: wAVUTI

No comments :

Post a Comment