dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, September 12, 2014

CUF walalamikia Tume ya uchaguzi ugawaji wa majimbo

 Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akizugumza na Waandishi wa Habari kuhusiana Kuilalamikia Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC juu ya upitiaji, ugawaji na ubadilishaji  upya wa Majimbo na Wadi za uchaguzi Zanzibar.

  Mwandishi wa Habari wa Channel Ten Munir Zakaria akimuliza  swali  Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui. 
Naibu Katibu Mkuu CUF Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akisisitiza jambo alipokuwa akijibu maswali ya Waandishi wa Habari, wa kwanza (kushaoto) ni Mkurugenzi wa Habari na Uenezi  wa CUF Zanzibar Salim Bimani  na wapili (kulia) ni Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa  Omar Ali Shehe.
Picha na Jamila Abdalla-Maelezo Zanzibar

Mwashungi Tahir
 
Chama cha Wananchi CUF kimeishauri Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC kuzingatia matakwa ya Katiba na kufanya kazi zake kwa uadilifu katika kusimamia zoezi la Uongezaji na Upunguzaji wa Mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi.
 
Aidha CUF kimeitaka Tume hiyo kutokupokea Maagizo yoyote nje ya Mamlaka yake ili kuimarisha ustawi nzuri wa Demokrasia ndani ya Zanzibar.
 
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari katika Ofisi ya CUF iliyopo Vuga mjini Zanzibar.
 
Mazroui amesema ZEC haipaswi kuangalia kigezo kimoja tu cha Takwimu ya Wakaazi katika Jimbo husika badala yake waangalie na vigezo vingine katika kugawa Majimbo.
 
Amedai kuwa ZEC Inapaswa kuzingatia kuwa kuwepo kwa Malalamiko ya muda mrefu ya Wadau wa Uchaguzi juu ya Utaratibu mbovu wa Ugawaji wa Majimbo Zanzibar kulipelekea uvunjifu wa Amani kutokana na baadhi ya Wananchi kutoridhika na hali hiyo.
 
Aidha Mazrui ameitaka tume ya uchaguzi kuzingatia mazingira ya amani na maelewano yaliyopo na kutokuwa taasisi ambayo itakuwa chanzo cha vurugu na mifarakano katika nchi.
 
“Tunaiomba ZEC ifahamu kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ipo na inaendelea kufanya kazi zake Vyema hivyo ZEC isijaribu kuwa kichocheo cha kuivuruga Serikali hiyo” Alisema Mazrou.
 
Hivi karibuni tume ya Uchaguzi ZEC ilitoa Taarifa ya kuyagawa Majimbo ya Uchaguzi lakini Chama cha Wananchi CUF kimedai Ugawaji wa Majimbo hayo umefanywa kisiasa bila kuangalia hali halisi.
 
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

No comments :

Post a Comment