- WASHINGTON DC ATTORNEY GENERAL KUINGILIA KATI.
- ANAMAMLAKA KISHERIA KUCHUNGUZA UFISADI
- WATAKAOBAINIKA KUITUMIA JUMUIYA KWA MASLAHI BINAFSI KUCHUKULIWA HATUA KALI ZA KISHERIA.
- IRS KUSHIRIKI KATIKA UCHUNGUZI HUO
Bodi Memba wa ATC akimtisha Libe kwa kumtumbulia macho katika mkutano wa juzi!
Mgogoro ulioikumba
jumuiya hii baada ya wachache kuitumia kwa maslahi binafsi umechukua sura mpya
baada ya Attorney General wa Washington DC ilikosajiliwa jumuiya hii na mwenye
mamlaka kisheria ya udhibiti wa jumuiya kama hizi kufanya kazi yake ya uchunguzi
zidi ya ubadhirifu na ufisadi unaozikumba jumuiya, taasisi za kidini na vikundi
mbalimbali vilivyosajiliwa chini yake kwa chatter ya " for nonprofit
organization and 501(3)c - Tax Exemption". Hali imekuwa sugu kwa vikundi
vingi na wahusika wa ubadhirifu wameshitakiwa na kupewa hadhabu kali sana
pamoja na vifungo kati ya mwaka mmoja na kuendelea. Moja ya mashariti ya
usajiri wa jumuiya hizi ni kuzingatia kanuni na sheria zinazotoa muongozo wa
kazi zake, hivyo kutozifuata upelekea jumuiya kufungiwa na watekelezaji wake
kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Vijana wa kikundi cha Nyarugusu wakiwa kazini! |
Uongozi unawajibika
kuwajulisha wanachama taarifa za fedha na miradi iliyopo, pia kutunza
kumbukumbu na kuwaziweka wazi kwa wanachama wakati wote.
Pia ni wajibu wao kuipa taarifa mara kwa mara ofisi ya Attorney General ili kudumisha usajiri wa jumuiya husika. Taarifa za mapato na misamaha ya kodi hupelekwa Idara ya kodi IRS sharti muhimu ili jumuia husika iendelee kuwa na kibari cha msamaha wa kodi "Tax Exemption for nonprofit making Organization/Corporation" kanuni ijulikanayo kama 501(c) 3. Hatua hii itamaliza mzizi wa fitina na kusafisha wale wote waliohusika kuihujumu jumuiya kwa kipindi kirefu. Watu hawa wametumia mbinu maksudi kuwagawa wanachama kidini, kiitikadi, kuwazuia wanachama kuona rekodi za mikutano, miradi na fedha.

Hatua ya baadhi ya
wanachama kwenda mahakamani na sasa wengine kumuhusisha Attorney General
itakuwa ni hatua muafaka katika kutatua mgogoro huu uanaozidi kukomaa kila
kukicha na itakuwa fundisho kwa vizazi vijavyo na wale wachache wanaopenda
kuishi nchini hapa kwa kutumia migongo ya walio wengi ili kusukuma agenda ovu
ya ufisadi.
Chanzo: Swahilivilla
No comments :
Post a Comment