Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, September 11, 2014

URAIA PACHA: AHSANTE BABA ZAHORO LYASUKA - WAFAHAMISHE WASIOELEWA!!!

 immigrt12
 Ofisa mstaafu Uhamiaji atoa angalizo uraia pacha
Na Restuta James

Ofisa mstaafu katika Idara ya Uhamiaji, Zahoro Lyasuka, ameliomba Bunge Maalum la Katiba kuingiza kipengele kinachoruhusu uraia pacha kwenye Katiba ijayo ili kuwasaidia Watanzania waishio nje ya nchi.
Akizungumza na NIPASHE, Lyasuka ambaye ni mtaalam wa ukaguzi Uhamiaji, alisema haoni uhusiano baina ya uzalendo, usalama wa Taifa na uraia wa nchi mbili.
Alisema hata hapa nchini wapo raia (viongozi), wasio na uraia wa nchi mbili, lakini wameliingiza Taifa kwenye hasara kubwa.
“Ukizungumzia masuala ya kuhatarisha usalama; ubalozi wa Marekani ulilipuliwa mwaka 1998, je, aliyepiga mabomu alikuwa na uraia wa nchi mbili?” alihoji.
Alisema uhalifu ni kosa kama makosa mengine. “Tusije tukachanganya uraia wa nchi mbili na uhalifu, hivi ni vitu viwili tofauti,” alisema.
Alisema: “Kusema uraia wa nchi utahatarisha usalama wa nchi siyo kweli.

Uzalendo wa mtu upo moyoni mwa mtu bila kujali ana uraia wa nchi ngapi. Mtu anaweza akawa hapa Dar es Salaam au kijijini na akahatarisha usalama.”
Alisema kuhatarisha usalama ni kosa kisheria na kwamba mtu anayefanya hivyo anapaswa kushughulikiwa kwa mujibu wa taratibu na sheria.
Alisema Bunge Maalum la Katiba litafanya makosa makubwa kama litawanyima haki ya uraia Watanzania waishio nje ya nchi ambao wamepata uraia katika nchi wanazoishi.
Alisema kinachopaswa kutazamwa ni aina gani ya uraia akifafanua kuwa wanapaswa kupewa uraia pacha ni Watanzania wa asili siyo raia wa nje waliopewa uraia.
Lyasuka alisema Watanzania wengi walio nje ya nchi wapo kimkakati na kwamba fedha wanazopata huko watakuja kuwekeza au kujenga nyumbani, hivyo wasipopewa uraia wa Tanzania watashindwa kutimiza malengo yao.
Alisema hata sheria ya Uhamiaji ya mwaka 1995, kifungu cha 14, kinazuia mtu yeyote akiwamo Waziri wa Mambo ya Ndani kunyang’anya uraia kwa Mtanzania wa asili lakini katika hali ya kushangaza Bunge Maalum linataka kuwafutia haki hiyo.
Suala la uraia pacha liliwekwa kwenye rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba, lakini Bunge Maalum la Katiba limefuta ibara hiyo baada ya serikali kueleza athari za kiuchumi na kiusalama kama jambo hilo litaruhusiwa kikatiba.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment