Jengo la Mkutano waTatu wa Kimatifa wa Nchi za Visiwa linaloitwa Apia kama linavyoonekanwa mkutano huo umejumuisha nchi mbali mbali ikiwemo Zanzibar.
Rais wa Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa nchi za Visiwa Bw.Tuiluepa Sailele Malielegaoi,akitoa hotuba yake katika mkutano huo wenye malengo ya kuleta maendeleo ya nchi ulioanza leo katika jengo la Apia nchini Samoa utakaoendelea kwa siku tatu kwa udhamini wa UN (kulia) Katibu Mkuu wa UN Ban Ki-moon na Bw. Wu Hongbo Katibu Mkuu wa Mkutano huo,(katikati).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hotuba yake katika Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa nchi za Visiwa wenye malengo ya kuleta maendeleo ulioanza leo katika jengo la Apia nchini Samoa akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk,Jakaya Mrisho Kikwete,mkutano huo wa kwa siku nne umedhamini wa UN.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Bw.Ban Ki-moon akitoa hotuba yake katika Mkutano wa tatu wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa wenye malengo ya kuleta maendeleo ulioanza leo katika jengo la Apia nchini Samoa utakaoendelea kwa siku nne kwa udhamini wa UN.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa nchi za Visiwa wenye malengo ya kuleta maendeleo ya nchi ulioanza leo katika jengo la Apia nchini Samoa kwa uliodhamini wa UN wakifuatilia kwa makini Mkutano huo ukiendelea kwa hotuba mbali mbali za Viongozi.
Rais wa Serikali ya Visiwa vya Comoro Ikililou Dhoinine akitoa hotuba yake katika mkutano wa tatu wa Kimataifa wa nchi za Visiwa wenye malengo ya kuleta maendeleo ulioanza leo katika jengo la Apia nchini Samoa utakaoendelea kwa siku nne kwa udhamini wa UN (kulia) ni Bw. Wu Hongbo Katibu Mkuu wa Mkutano.
Picha ya pamoja ya Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika Mkutano wa tatu wa Kimataifawa nchi za Visiwa wenye malengo ya kuleta maendeleo ya nchi ulioanza leo katika jengo la Apia nchini Samoa uliodhaminiwa na UN. [Picha na Ramadhan Othman Samoa.]
Chanzo; ZanziNews
No comments :
Post a Comment