Waziri wa Ardhi Maakazi Maji na Nishati Mhe. Ramadhani Shaban, akizindua ununuzi wa Umeme wa Tukuza kupitia Mtandao wa Zantel wa EZYPESA, akiweka namba katika mita ya tukuza wakati wa uzinduzi huo, akisomewa namba hizo na Mkurugenzi Fedha kupitia Mtandao Ndg. Hashim Mukudi.imefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Zanzibar.
Waziri wa Ardhi Maakaazi Maji na Nishati Mhe. Ramadhani Shaban, akipiga makofi baada ya kuzindua ununuzi wa Umeme wa Tukuza kupitia Mtandao wa Zantel wa EZYPESA, uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Zanzibar.
Waheshimiwa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo kutoka kulia Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Mkurugenzi Mtendaji wa ZANTEL Ndg.Pratap Ghose, Waziri wa Ardhi Maakazi Nishati na Maji Mhe Ramadhan Abdalla Shaban, Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar Ndg.Hassan Mbarouk, Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mhe. Juma Duni Haji na Waziri wa Afya Mhe Rashid Seif Suleiman.
Mawaziri na Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Umeme wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Kampuni ya Simu ya ZANTEL baada ya kuzindua ununuzi wa umeme kupiotia mtandao wa EZYPESA, uliozinduliwa na Waziri wa Ardhi Makaazi Nishati na Maji.Mhe. Ramadhani Abdalla Shabani
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ZANTEL Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Zatel baada ya uzinduzi wa Kununua Umeme kupitia EZYPESA, uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Grand Palace Malindi Zanzibar.
Chanzo: ZanziNews
No comments :
Post a Comment