Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, October 21, 2014

Mzee Moyo afichua siri


Mzee Moyo afichua siri
20, 2014 october
Madudu ya urais CCM haya hapa:-
Mzee Hassan Nassoro MOYO ameeleza jinsi alivyoshiriki kuinusuru znz kuingia kwenye umwagikaji wa DAMU mkubwa baada ya CCM kushindwa kwa mbali katika uchaguzi wa mwaka 2010.
MOYO asimulia alivyotumwa kumwangukia Maalim Seif akubali ushindi HARAMU wa CCM Zanzibar baada ya Rais wa Zanzibar Amani Karume na mwenyekiti wa CCM taifa Rais Jakaya Kikwete kumwagiza kufanya hivyo.
“Mimi ndiye niliyetumwa na mwenyekiti wa CCM(kikwete) na Rais Karume akafanye kile ambacho anaamini ndiyo kilichoviepusha visiwa hivyo na machafuko baada ya mwenyekiti wa CCM taifa na Rais Karume kusema wako tayari kwa lolote lakini sio kumtangaza mshindi (Maalim Seif)”.
Akisimulia, MOYO ambaye ndiye alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya maridhiano ya watu sita znz alisema “saa chache kabla ya Tume ya uchaguzi znz kutangaza matokeo urais, alikutana na aliyekuwa mgombea wa urais wa Chama Cha Wananchi Cuf Maalim Seif Sharrif Hamad. Akisimulia kuhusu mkutano huo, MOYO alisema alikwenda kuonana na kiongozi huyo mwenye ushawishi mkubwa znz baada ya kuombwa na aliyekuwa Rais wa znz Amani Karume na mwenyekiti wa CCM taifa Rais Jakaya Kikwete.
“Siku ya kutangaza matokeo ya urais 2010 alikuja kijana hapa kwangu USIKU Eddy Riyami majira ya 10:00 alfajir akasema ametumwa na Rais Amani Karume nikamuone Maalim Self, nikauliza kunanini, nikazungumze nae nini? Nikamuliza Eddy je tumeshindwa? akatabasamu (smile) akasema NDIYO tumeshindwa” Mimi ni mtu mzima, nikasema siondoki mpaka nisali, nikasali mpaka saa 11:30 tukaondoka na gari yake mpaka kule.
MOYO ambaye alikuwa mmoja wa Wazanzibar waliounda Baraza la kwanza la Mapinduzi chini ya Hayati Abedi Karume anaamini kwamba ushawishi wake kwa Maalim Seif ndio hatimaye uliosaidia kuviokoa visiwa vya Zanzibar na umwagikaji mkubwa wa DAMU hasa kutokana na msimamo wa CCM kuwa wapo tayari kwa lolote lakini hawawezi kumtangaza mshindi halali (Maalim Seif).Hatimaye kutangazwa kwa matokeo yaliyompa ushindi Mhe Shein ushindi wa 50.1 dhidi ya 49. uliotangazwa kupata Maalim Seif.
“Tukaonana na Maalim Seif na tulikutana na vijana wengi wamekusanyika. Gari tuliacha msikitini kule, baadhi ya vijana wakaniuliza Moyo unakwenda kupigania serikali yetu? Ndiyo mara ya kwanza naingia kwenye ofisi za Cuf Mlandege” alisema Moyo
Akizungumza hali ilivyokuwa katika ofisi za CUF, alisema aliwakuta baadhi ya makada wa chama hicho akiwemo Juma Duni Haji, Ismail Jussa, Machano Khamis, na Ally Haji pamoja na Maalim Seif .
MOYO alisema kwa sababu hakutaka maongezi yake na Seif yasambae aliwaomba wawapishe isipokuwa Jussa na Eddy . “Nilizungumza na Maalim Seif kwa saa moja na nusu huku yeye akiwa ananitazama tu bila kusema lolote”
“Mimi sisemi kwa kubahatisha, sio mtu mwa kubabaisha, wala siogopi sikuumbwa kuogopa mimi”
Baada ya kumaliza nikamwambia, aliyonituma ndugu yako Amani Karume kwamba yakitangazwa matokeo jioni ya leo uyakubali…… ..Endelea kufuatilia sehemu ya pili kesho
Chanzo: Mtanzania

No comments :

Post a Comment