Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, October 31, 2014

PINDA AWALAZA MKUTANONI WATANZANIA WANAOISHI OMAN!

Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambae aliwalaza Watanzania wanaoishi 
Oman katika mkutano nao huko Muscat hivi majuzi.

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe Mizengo Kayanza Peter Pinda alizungumza na Watanzania waishio nchini Oman wakati akihitimisha ziara yake nchini humo Oktoba 29, 2014. Katika mazungumzo hayo alikuwepo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maalim Mahadhi  pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe Ali Ahmed Saleh.

Hakijulikani kitu gani kilichowafanya baadhi ya Watanzania kulala katika mazungumzo hayo. Labda zimewatosha hadithi zile zile za siku zote za CCM, huku nchi ikiendelea kuliwa na wakubwa kutokana na corruption iliyoenea katika kila pembe ya nchi!

Baadhi ya watanzania waishio Oman wakimsikiliza Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati alipowahutubia kwenye hoteli ya Al Bustan, mjini Muscut, Oktoba 29, 2014, huku Watanzania wengine wakiwa wamelala fo-fo-fo na wengine wakishughulikia simu zao za mikononi! 
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


1 comment :

  1. Kiasi Waomani walale mkutanoni, kwasababu wao sio wajinga. Pinda anafikiri Waomani wa leo ndio wale Wamanga tongo? Anataka kuwakopa TShs bilioni 200 kuziba wizi wao huko IPTL watakubali wapi?
    Washikilieni hao hao EU wakupeni hizo pesa walizozizuwia za TShs trilioni moja. Waomani hawapo tayari kukupeni mkopo ili pesa ziingie chooni kwenye lindi. Kwahivyo hio kulala kwa huyo mama hapo juu na wengine waliokuwa wakisinzia mkutanoni kunasema mengi!
    Baada ya kushughulikia pesa bilioni 200 zimekuenda wapi mbio mbio wanataka kukopa, kwasababu wanajua zilienda wapi!

    ReplyDelete