Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, October 28, 2014

Yaliojiri Mkutano wa CCM Kibanda Maiti Zanzibar

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipokea risala ya Vijana wa UVCCM baada ya kusomwa wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM katika viwanja vya kibanda maiti Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia WanaCCM katika viwanja vya kibandamati na kuwaonesha Rasimu ya Katiba iliowakilishwa katika Bunge la Katiba na kutoa Mapendekezo ya Katiba Mpya ilioungwa na Wajumbe wa Bunge la Katiba Mjini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akionesha Katiba Mpya ilopendekezwa na Wajumbe wa Bunge la Katiba Tanzania hivi karibuni na kukabidhiwa Marais wawili wa Tanzania na Zanzibar katika viwanja vya mpira Dodoma, akiwaonesha wananchi waliohudhuria katika mkutano wa hadhara na kuwataka kuipigia kura ya ndio wakati ukifika wa kura ya maoni.mkutano huo umefanyika katika viwanja vya kibanda maiti Zanzibar.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akizungumza na Wananchi na Wanachama wa CCM wakati wa Mkutano wa hadhara katika viwanja vya kibandamaiti Zanzibar. 
Viongozi wa CCM wakifuatilia mkutano wa hadhara wa CCM ulioandaliwa na Afisi Kuu ya CCM Zanzibar katika viwanja vya kibanda maiti Zanzibar. 
                    Wanachama wa CCM wakiwa katika viwanja vya mkutano wakishangilia.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Ndg Borafi Silima akihutubia katika mkutano huo katika viwanja vya kibanda maiti Zanzibar.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakimshangilia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika mkutano huo katika viwanja vya kibanda maiti Zanzibar.

Viongozi wa meza Kuu wakimsikiliza Muasisi wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Mzee Hamid Ameir akitowa historia ya Zanzibar ilikotoka hadi leo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya kibanda maiti Zanzibar na kuzungumza na WanaCCM na Wananchi kuhusiana Zanzibar.
Musisi wa Mapinduzi na Chama cha Mapinduzi Mzere Hamid Ameir, akizungumza na WanaCCM na Wananchi wa Zanzibar katika viwanja vya kibandamaiti Zanzibar kuzungumzia Zanzibar na Katiba Mpya ya Tanzania.  
Aliyekuwa Mjumbe wa Bunge la Katiba Tanzania Mhe. Haidar Madoeya, akizungumzai Katika Mpya iliopendekezwa, wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM Kibanda maiti Zanzibar,akiwa Mjumbe aliowakisha Jumuiya ya Watu Wenye Ulemavu Zanzibar katika bunge hilo Dodoma. 
Aliyekuwa Mjumbe wa Bunge la Katiba Tanzania kutoka Pemba.Mhe.Khadija Nassor Abdi, akizungumzia Katibac Mpya iliopendekezwa baadhi ya Vifungu vya Katiba hiyo kwa Wananchi na WanaCCM waliohudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya kibandamaiti Zanzibar. 
Aliyekuwa Mjumbe wa Bunge la Katiba Tanzania na Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Asha Bakari, akihutubia wakati wa mkutano huo na kuonesha Katiba ya Tanzania iliopendekezwa na kusoma baadhi ya vipengele kwa Wananchi wa Zanzibar katika viwanja kibandamaiti.   
Mwakilishi wa Tumbatu na alikuwa mjumbe wa Bunge la Katiba Tanzania akiwahutubia WanaCCM na Wananchi wa Zanzibar kuhusiana na mapendekezo ya Katiba mpya iliowasilishwa kwa Rais wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, mjini Dodoma.  
Wanachama wa CCM wakishangiliwa wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika kibanda maiti Zanzibar
Waziri wa Fedha Tanzania na aliyekuwa Mjumbe wa Bunge la Katiba Mhe. Saada Mkuya akizungumza baadhi ya vifungu vya Katiba vinavyozungumzia Fedha, wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika viwanja vya kibandamaiti Zanzibar.akivichambua vifungu hivyo wakati wa mkutano huo. 

Vijana wa UVCCM wakishangilia wakati wa mkutano wa CCM kibandamaiti wakishangilia kwa aina yake. 


Wananchi wakiwa katika viwanja vya mkutano vya kibandamaiti wakifuatilia mkutano huo uliohutubiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar katika viwanja vya kibandamaiti Zanzibar. 
Shekh. akisoma dua baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya kibandamaiti Zanzibar. 
Wananchi na Viongozi wa CCM wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliofanika viwanja vya kibandamaiti Zanzibar.

Chanzo: ZanziNews

No comments :

Post a Comment