dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, December 13, 2014

MWAKILISHI WA UNICEF AKUTANA NA DK.SHEIN.

Rais wa Zanzibar na Mqwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwakilishi Mkaazi wa UNICEF Nchini  Tanzania Dr.Jama Gulaid alipofika Ikulu Mjini Unguja akiwa na ujumbe aliofuatana nao leo.

 Rais wa Zanzibar na Mqwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza  na Mwakilishi Mkaazi wa UNICEF Nchini  Tanzania Dr.Jama Gulaid alipofika Ikulu Mjini Unguja leo.[Picha na Ikulu.]

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
  Zanzibar                                                                                                           12.12.2014
---
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto ulimwenguni (UNICEF) limepongeza juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kupiga vita udhalilishaji wa watoto pamoja na mafanikio yaliopatikana katika utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto hapa nchini.

Pongezi hizo zimetolewa leo na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto Ulimwenguni (UNICEF)  nchini Tanzania Mhe. Jama Gulaid wakati alipofanya mazunbgumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein Ikulu mjini Zanzibar.

Katika maelezo yake Mwakilishi huyo wa UNICEF hapa nchini alieleza kuwa Shirika hilo limevutiwa na juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Ungozi wa Dk. Shein kutekeleza kwa vitendo Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto na kuahidi kuendelea kuziunga mkono juhudi hizo.Alisema kuwa mafanikio makubwa yameweza kupatikanwa hapa nchini ambapo hivi sasa watoto wengi wamekuwa wakipata haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na fursa ya kujiunga skuli na kupata haki yao ya elimu pamoja na huduma za afya na nyenginezo.

Aidha, Mhe. Gulaid alitumia fursa hiyo kuwapongeza wazazi kwa juhudi zao hizo za kuwapatia elimu watoto kwa kushirikiana na serikali yao katika kuwatunza na kuwalinda watoto pamoja na kupongeza juhudi za serikali katika kupunguza vifo vya akina mama na watoto vilivyotokana na maradhi mbali mbali yakiwemo Malaria.

“Leo vifo vya watoto wachanga vimepungua, watoto wengi zaidi wanakwenda skuli, watoto wanahifadhiwa zaidi na kupatiwa msaada wa kisheria pale unapohitajika..hongera sana pamoja na Wazanzibari wote kwa ujumla”,alisema Gulaid.

Mhe. Gulaid ambaye alifuatana na watendaji wa Shirika hilo wanaofanya kazi zao hapa Zanzibar alisema kuwa uzinduzi wa Kampeni ya kupiga vita ukatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto uliofanywa hivi karibuni na Dk. Shein umedhihirisha wazi jinsi Serikali inavyowajali watoto wka kuamini kwamba suala zima la udhalilishaji kwa watoto litapungua ama kuondoshwa kabisa.

Pamoja na hayo, Mwakilishi huyo alieleza kuwa katika kutekeleza wasia aliowapa Mhe. Rais wakati walipokutana mwaka jana  kwa kuangalia uwezekano wa kuwawezesha wananchi, alieleza kuwa tayari wameshakushanya rasilimali za kutosha katika kusaidia afya ya mama na mtoto, elimu pamoja na uhifadhi wa mtoto.

Alieleza kuwa katika kuunga mkono katika maeneo hayo makubwa matatu tayari shirika lake limeshakusanya rasilimali za kutosha ambapo kwa upande wa afya ya mama na mtoto shirika hilo limeahidi Dola za Kimarekani milioni 12 na Dola milioni 6.5 kwa elimu na Dola 15 katika kupambana na maambukizo ya virusi vya ukimwi.

Aidha, Mwakilishi huyo alisema kuwa katika kuwajengea watendaji uwezo Shirika hilo litaimarisha kituo cha Afya cha Kivunge ili kipate uwezo wa kutoa huduma bora kwa watu zaidi ya laki mbli wanaoishi katika Mkoa wa Kaskazini Unguja. Kwa upande wa sekta ya elimu aliwataka wazazi kuwaandikisha watoto wao skuli kwa wakati.

Nae Dk. Shein kwa upande wake alieleza kuwa UNICEF ni miongoni mwa mashirika ya Umoja wa Mataifa ambalo limekuwa likiiunga mkono Zanzibar kwa kipindi kirefu na kulipongeza kwa misaada yake mbali mbali kwa Zanzibar pamoja na Tanzania Bara.

Dk. Shein alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imedhamiria kwa dhati kupunguza ama kuondosha kabisa udhalilishaji wa wanawake na watoto na uzinduzi wa Kampeni ya kupiga vita masuala hayo uatasaidia kwa kiasi kikubwa.

Aidha, Dk. Shein ameeleza kufarajika kwake na Jumuiya za Kimataifa kuunga mkono Kampeni hiyo  na kueleza kuwa kazi kubwa iliyopo mbele ni kuielimisha jamii kwani wengi wanaofanya vitendo hivyo huwa katika familia.

Dk. Shein alisisitiza kuwa Serikali imeamua kuimarisha jitihada zake katika kufanya utafiti baina ya nyumba na nyumba ili kuweza kupata takwimu za uhakika.

Aidha, Dk. Shein amepongeza azma ya Shirika hilo la kuwaongezea uwezo watendaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na kusaidia fedha katika kuendeleza huduma za afya ya mama na mtoto, elimu pamoja na uhifadhi wa mtoto.

Dk. Shein alieleza  mafanikio yaliopatika hapa Zanzibar katika sekta ya afya pamoja na sekta ya elimu na kueleza kuwa hivi sasa si zaidi ya kilomita tano tayari kumekwua na kituo cha afya ambapo changamoto kubwa iliyopo hivi sasa ni uhaba wa dawa.

Kwa upande wa sekta ya elimu alisema kuwa Serikali kupitia Wizara yake husika imekuwa ikifanya jitihada katika kuhakikisha watoto waliofika umri wa kuandikishwa skuli wanapata fursa hiyo na kueleza juhudi zinazofnywa katika kuimarisha miundombinu ya elimu.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar                

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk


No comments :

Post a Comment