Ujumbe wa wadi za Makunduchi umetembelea shughuli za kufuma kwa mkono zinazoendeshwa na akinamama wa Manispa ya Sundsvall Sweden. Miongoni mwa kazi za ujasiriamali zanazotegemewa kufanjwa na akinamama wa wadi za Makunduchi ni kufuma. Kwa mujibu wa mazungumzo yaliyofanjwa na diwani Zawadi na wenyeji wake akinamama wa Makunduchi watapatiwa soko la kazi zao za kufuma katika manispaa ya Sundsvall. Katika picha kutoka kushoto ni mwalimu Hafifth Hamid, diwani Zawadi, mwalimu Kinore na ndugu Mohd Simba.
Mvuvi huyu yuko juu ya ziwa lenye maji ya kina kirefu ambalo limegeuka barafu ngumu sehemu ya juu. Kuvua katika ziwa hili unahitaji kuwa na 'drill' inayoonekana kwenye picha kwa ajili ya kufanya tundu hadi kwenye maji na hatimaye unapitisha mshipi wenye chambo.
Ujumbe wa Makunduchi baada ya kuangalia uvuvi unaoendeshwa kwenye ziwa lililogeuka kuwa barafu ngumu sehemu ya juu katika kipindi hiki cha baridi kali. Kutoka kushoto ni mratibu wa safari ndugu Mohamed Muombwa, mwalimu mkuu wa skuli ya Sekondari ya Makunduchi ndugu Kinore, mwalimu Hafidh Hamid, bi, Christin, Mohd Simba na diwani Zawadi.
No comments :
Post a Comment