Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, December 17, 2014

Wateja wa Zantel na Tigo Sasa Kufurahia Huduma Salama na Yauhakika ya Kutumiana Fedha kwenye Mitandao yao kwa 100%.

Watendaji wa Kampuni za Simu za Zantel na Tigo wakiwa katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace kuitambulisha huduma ya kutuma fedha kupitia mitandao hiyo bila ya gharama kubwa hutumika kwa gharaza za kawaida za makampuni hayo, kutoka kulia Mkurugenzi wa Huduma za Fedha Zantel Mr.Hashim Mukudi, Mkurugenzi Biashara Zantel Mr Mohammed Khamis Mussa Baucha, Mkuu Kitengo cha Huduma za Fedha Tigo Mr.Andrew Hodgson na Meneja Chapa Mr. William Mpinga.
Mkurugenzi Biashara Zantel Mr Mohammed Khamis Mussa (Baucha) akizungumza na waandishi wa habari uzinduzi wa huduma za utumiaji wa huduma ya Fedha kwa mitandao ya Zantel na Tigo kwa wateja wa makampuni hayo kuweza kutuma fedha kwa mteja wa Tigo kwenda kwa Zantel kwa kiwango cha gharama cha kawaida kama unavyotuma fedha kwenda kwa Zantel kwa Zatel na kwa Tigo hali kadhalika, uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Malindi Zanzibar. 
 Mkuu Kitengo cha Huduma za Fedha Tigo Mr.Andrew Hodgson, akizungumza wakati wa uzinduzi huo katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Malindi Zanzibar, kuwajulisha wateja wa Togo wanaweza kutuma fedha kwenda Zantel bila ya gharama kubwa makato yake kama unavyotuma fedha kwenda Tigo kwa Tigo. 
Mkurugenzi wa Huduma za Fedha Zantel Mr.Hashim Mukudi, akifafanua jambo wakati wa uzinduzi huo kwa waandishi wa habari kuhusiana na huduma hiyo ya ushirikiano na kampuni ya Tigo kuweza kutumia viwango sawa wakati wa kutumiana fedha mteja wa Zantel kwenda Tigo.
Meneja Chapa Mr. William Mpinga, akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi huo kuhusiana na huduma hiyo kwa wateja wa Tigo kuweza kutuma fedha kwenda Zantel.




Mkurugenzi Huduma ya Fedha Zantel kulia Mr.Hashim Mukudi, wakipongezana na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha Tigo Mr Andrew Hodgson, baada ya hafla ya kuitambulisha huduma hiyo kwa Wananchi wa Zanzibar kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Malindi Zanzibar leo.kwa kutuma fedha kupitia mitandao ya Zantel na Tigo kwa kutumia gharama za kawaida za kampuni hizo.
Mkurugenzi Huduma ya Fedha Zantel kulia Mr.Hashim Mukudi, wakipongezana na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha Tigo Mr Andrew Hodgson, baada ya hafla ya kuitambulisha huduma ya kutuma fedha kupitia mitandao ya Zantel na Tigo kwa kutumia gharama ya kawaida ya kampuni hizo inayokatwa kwa kutuma fedha kwenda Zantel na Zantel, kulia Mkurugenzi wa Miradi wa Zantel Bi Shihuna Kassim na Mkurugenzi Biashara Zantel Mr. Mohammed Khamiss Mussa na kushoto Meneja Chapa wa Togo Mr William Mpinga, wakifurahia udugu huu baada ya kuzungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Grand Palace Malindi Zanzibar.
Viongozi wa Kamuni za Simu za Zantel na Tigo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuutambulisha uhusiano wao kwa Wateja wao kupata huduma ya kutumiana Fedha kupitia mitandao hiyo. utambulisho huo umefanyika katika Hoteli ya Grand Palace Malindi Zanzibar.

No comments :

Post a Comment