Mr President - hii kuumwa na kichwa umejitakia mwenyewe
kwa kujizungusha na wezi wasioitakia jema nchi yetu!
(Zanzibar) – Inasemekana
kuwa baadhi ya Wazanzibari hivi karibuni watakutana na Balozi wa
Finland katika Tanzania Bibi Sinikka Antila ambae ni Mwenyekiti wa EU Budget
Support Development Partners (DP) pamoja na Balozi wa Marekani katika Tanzania
Bwana Mark Childress. Mkutano huo utakuwa na nia ya kuiomba EU pamoja na Serikali ya Marekani chini ya mpango wake wa Millennium Challenge Corporation (MCC) ili Zanzibar ipatiwe sehemu yake ya 4.5% ya pesa ambazo Serikali ya Muungano itazikosa, kama Rais wa Jamhuri ya Tanzania atashindwa kuchukuwa hatua madhubuti na kali ambazo zitawafanya wahisani wa EU na Serikali ya Marekani kubadilisha misimamo yao juu ya hii kasheshe ya wizi kutoka katika Akaunti ya Escrow ya Tegeta.
Wazanzibari hao ambao hawajulikani ni wachama gani wanasema hizi ni pesa nyingi sana kuzikosa na
kama Serikali ya Muungano haitojali kwa kukosa kutoa adhabu kali kwa hawa wezi ili
wahisani wabadilishe mawazo yao, basi Zanzibar iombe kwa wahisani sehemu yake ya 4.5% ambayo
ingepata kutoka kwa Serikali ya Muungano kama wizi wa Escrow usingelikuwepo,
kwaajili ya maendeleo ya Zanzibar.
Ambassador Sinikka Antila of the Embassy of Finland in Tanzania with Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation in 2012 in his office in Dar es Salaam.
MCC peke yake ilipanga kuipa Tanzania baina ya $450-700
millions na EU $489 millions baada ya kuisha kutanguliza kutoa $69 millions mapema mwaka huu.
Inafahamika kuwa katika miaka 5 iliyopita Tanzania ilitegemea sana juu ya $698
millions iliyopokea kupitia huu mpango wa MCC kwaajili ya miradi yake ya
kusambaza umeme na maji safi nchini. Zikikosekana pesa hizi za MCC kasi ya miradi
hii ambayo inawasaidia sana wananchi wengi hasa wa vijijini itapungua.
“ Kwa kweli tunahakika kuwa wahisani hawatorejea nyuma,
kwasababu hatua atakazozichukuwa Rais wetu tayari zinajulikana, nazo ni:
Kwanza, atawataka wote waliopewa pesa kiholela kutoka Akaunti ya Escrow
wazirejeshe kwa muda wa mwezi mmoja. Pili, atawatoa Serikalini wale wote
waliohusika na wizi huu, kama mapendekezo ya Bunge yalivyotaka, lakini, Rais
hatopendekeza kuchukuliwa kwa hatua za kisheria kwa hawa wezi right away,
isipokuwa Rais atatamka kuwa uchunguzi unaendelea na kama pakionekana kuwa
sheria za nchi zilivunjwa basi wahusika watapelekwa mahakamni. Hapo ndipo
itakapomalizikia kesi hii na hakuna hatua zozote za kisheria
zitakazochukuliwa huko mbele”, alielezea msomi mmoja ambae anafuatilia hii
habari ya Akaunti ya Escrow kwa karibu sana.
“Kama wezi hawatochukuliwa
hatua za kisheria right away wahisani hawatoridhika, kwani watadhania kuwa kuna
mikono mingi iliohusika na wizi huu na ambayo inafichwa,” aliendelea.
“ Kwa upande mwengine, kama hatua za kisheria
zitachukuliwa na Rais, basi huenda zikafichua mambo ambayo itaifanya Serikali ya
Muungano kutikisika na CCM kubwagwa chini na kwahivyo hatua kama hizo Rais hatozichukuwa
”, aliendelea mzungumzaji huyo.
Walipoulizwa baadhi ya wachunguzi wa siasa wa mjini DSM
kuhusu uwezekano wa Zanzibar kuomba 4.5% yao kutokana na msaada wa EU na MCC,
wengi walisema kuwa hio ni haki yao Wazanzibari. “ Misaada yote inayokuja kwa
jina la Serikali ya Muungano, Zanzibar inayo 4.5%, japokuwa wakati mwengine
hatuwapi kitu. Lao kubwa Zanzibar ni kuifahamisha EU na Serikali ya Marekani kuwa wao hawamo katika
wizi uliotokea na kuwa hakuna Mzanzibari hata mmoja – kuanzia wanasiasa, mawaziri, majaji
au mapadri Wa Zanzibar ambao walihusika na wizi huu na kwahivyo wasitiwe Wazanzibari adabu ya
kunyimwa hii misaada”, alielezea mchunguzi mmoja wa siasa ambae hakutaka jina
lake litajwe.
Akaendelea kusema kuwa, “ Sio haki kuwa kuiba aibe Kaka na adabu atiwe Kaka pamoja na mdogo wake,
wakati mdogo wake wala hakuhusika na huo wizi. Kwahivyo, kama Rais
atashindwa kuonesha kuwa havumilii magendo, rushwa na wizi wa aina yoyote
ile nchini, basi Zanzibar itakuwa na haki ya kuiomba EU na MCC ili ipatiwe 4.5%
ya misaada hio kama mambo yatakuenda kombo kama wengi tunavyodhania kutokana na
historia ya vita vyetu dhidi ya rushwa nchini”, alimalizia huyu gwiji wa siasa.
Kwa vyovyote vile, bado ni mapema sana kusema chochote
kwa sasa. La kuomba ni kuwa Rais wetu atatoa adhabu kali kwa wezi wote, kama vile kufungwa maisha na kuporwa mali zao zote - adhabu ambayo
itakuwa fundisho kwa wezi wengine. Hatuombi kuwa uroho wa wakubwa fulani wa kutaka kujilimbikizia mapesa kwa mabilioni kwa haraka haraka kutatukosesha maendeleo yetu wananchi wa kawaida katika nchi hii.
No comments :
Post a Comment