Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, February 25, 2015

Chenge afungua pazia kibano vigogo Escrow leo.

Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge.
 Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM) leo anatarajiwa kusimama mbele ya Baraza la Maadili kujibu tuhuma za kukiuka maadili ya uongozi kwa kujipatia Sh. bilioni 1.6, ambazo zinadaiwa kuwa ni sehemu ya mgawo wa zaidi ya Sh. bilioni 300 zilizochotwa kifisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
 
Pia Mbunge wa Muleba Kusini, Prof. Anna Tibaijuka (CCM), ambaye alivuliwa Uwaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, anatarajia kujibu tuhuma hizo kesho mbele ya baraza hilo kutokana naye kupata mgawo wa Sh. bilioni 1.6, ambazo nazo zinadaiwa kuwa ni sehemu ya fedha zilizokuwamo katika akaunti hiyo.
 
Wote wawili wanatuhumiwa kupata mgawo huo kupitia kwa mmiliki wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira.
 
Ratiba iliyotolewa na baraza hilo jijini Dar es Salaam inaonyesha kuwa Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (CCM), ambaye anatuhumiwa kupata mgawo wa Sh. milioni 40 kutoka katika fedha zilikuwa zimehifadhiwa katika akaunti hiyo, atahojiwa na baraza hilo, Jumatatu ijayo.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment