Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, February 25, 2015

Ngeleja: Mgawo wangu Akaunti ya Tegeta Escrow ni wa msaada

Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja.
 Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja (pichani), amesema mgawo wa Sh. milioni 40 anaodaiwa kupewa kutoka kwenye fedha zilizochotwa kifisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ulikuwa msaada wa kawaida kama ambavyo wabunge wengine wamekuwa wakipewa.
 
Alisema hakuna mbunge anayeweza kutekeleza miradi ya maendeleo katika jimbo lake bila misaada.
 
Ngeleja aliyasema hayo juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kamanga kata ya Nyamatongo wilayani humo wakati akiwashukuru wapigakura wake kwa ujasiri wao wa kumkingia kifua dhidi ya kashfa ya akaunti hiyo inayomkabili.
 
Alisema siyo dhambi kwa wadau wa maendeleo zikiwamo kampuni, marafiki na taasisi kuchangia fedha ili kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika majimbo yao.
 
Kutokana na hali hiyo, aliwashukuru wapigakura wake kwa kumkingia kifua dhidi ya shutuma zinazoelekezwa kwake kwa kuwa wanalitambua hilo.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment