Cha mgema hunywewa na mlevi
Msaada wa Chenge ‘watafunwa’
KWA UFUPI
Kutokana na kushindwa kusimamia msaada huo vizuri, wajanja wachache wamepata mwanya wa kuitafuna, hivyo vijiji hivyo kushindwa kufikia malengo.
Bariadi. Wakazi wa vijiji vya Girigu na Bunamhala wilayani Bariadi, wameulaumu uongozi wa kata na wa shule ya Sekondari Giriku kushindwa kusimamia michango ya ujenzi inayotolewa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge.
Kutokana na kushindwa kusimamia msaada huo vizuri, wajanja wachache wamepata mwanya wa kuitafuna, hivyo vijiji hivyo kushindwa kufikia malengo.
Wakazi hao walidia kuwa mabati yaliyotolewa hivi karibuni na mbunge huyo hayajulikana yaliko na kuzua maswali mengi.
Hali hiyo imewalazimu wananchi kuchanga fedha za kununua mabati kwa ajili ya kuezeka vyumba vya maabara vya shule hiyo.
Walisema hayo juzi wakati wa ziara ya mbunge huyo shuleni hapo kukagua ujenzi wa maabara, ambao awali alichangia bati 180 ambazo hazijulikani zilipo.
Akisoma taarifa ya ujenzi wa maabara hiyo, Mtendaji Kata ya Bunamhala, Neema Mapalala alisema mabati waliyokopeshwa na halmashauri bado hayajalipiwa na yale yaliyotolewa na Chenge hayajulikani yalipo.
“Mimi ni mgeni hapa, lakini ninapokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wakidai kuna michango mingi inayotolewa na mbunge ya kusaidia shule hii zikiwamo hizo bati 180 hazijulikani ziliko,” alisema Mapalala.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Robert Lweyo aliutaka uongozi wa kata utoe maelezo kuhusiana na mabati hayo.
“Ofisi ya Mkurugenzi inazo taarifa kuwa mmepokea bati 180 kutoka kwa mbunge...ziko wapi bati hizo,” alihoji Lweyo.
Naye Katibu wa mbunge huyo, Masunga Lyabuyenze alisema mabati hayo aliyapeleka shuleni hapo na kuyakabidhi kwa uongozi wa shule na kata na anashangazwa na taarifa za kutojulikana yalipo mabati hayo.
“Mimi ndiye niliyepeleka mabati hayo pamoja na Sh4 milioni kwa ajili ya gharama za uezekaji,” alisema Lyabuyenze
Aliongeza: “Nashangaa hapa tunaelezwa taarifa tofauti, kwamba bati hizo hazijulikani zilipo. Tunapata picha kuwa bati pamoja na pesa hizo zilimetafunwa na wajanja wachache wa shule na viongozi wa kata.
No comments :
Post a Comment