Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, February 26, 2015

Mama Mwanamwema Shein Akabidhi Vifaa Dunga, Madrasa Afisi ya CCM na Saccos ya Utawala Bora.

Mwanafunzi wa Madrasa Tauin Mwera akisoma Quran kabla ya kuaza kwa hafla hiyo, iliofanyika katika viwanja vya Afisi ya Mkoa wa Kusini Unguja.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Viongozi wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja alipowasili katika viwanja vya Afisi ya CCM Mkua wa Kusini Unguja kukabidhi Vifaa hivyo.
Mke wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiwa na Viongozi wa CCM wakati alipowasili katika viwanja vya Afisi ya CCM Mkoa wa Kusini Unguja Dunga.
MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein akimkabidhi Seti ya Vipaza sauti Katibu wa Madrasa ya Tauin Mwera Ndg Hamad Ali, makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya CCM dunga.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi Katibu wa Saccos ya Utawala Bora Seti ya Komputer na Fotokopi, kwa ajili ya matumizi ya Saccos hiyo makabidhiano hayo yamefanyika Dunga Wilaya ya Kati Unguja  
MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi seti ya Fotokopi Katibu wa CCM  Mkoa wa Kusinu Unguja Bi Sauda Ramadhani , kwa ajli ya Afisi ya CCM Mkoa wa Kusini Unguja. kwa ajili ya matumizi ya Afisi ya CCM Mkoa. 

   Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Bi Sauda Ramadhan, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Bi Najma Muntaza Jinga, akitowa maelezo kabla ya kumkaribisha Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, kuhutubia hafla hiyo baada ya kukabidhi vifaa kwa wahusika.

MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akitowa nasaha zake kwa Wananchi wa Vikundi vya Wanawake vya Ushirika katika viwanja vya CCM Dunga wakati wa kukabidhi Vifaa kwa Madrasa Tauin ya Mwera Afisi ya CCM Mkoa wa Kusini Unguja na Saccos ya Utawala Bora. Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya CCM Dunga.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kati Unguja wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein,akitowa nasaha zake kwa Wananchi wa Wilaya hiyo katika hafla ya kukabidhi vifaa kwa Madrasa, Afisi ya CCM Mkoa na Saccos ya Utawala Bora, hafla iliofanyika katika viwanja vya Afisi ya CCM Dunga Wilaya ya Kati Unguja.
Wanafunzi wa Madrasa Tauini Mwera wakiwa na Vifaa vyao baada ya kukabidhiwa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, madrasa hiyi imekabidhiwa seti ya vifaa vya kupazia sauti kutumia wakati wa sherehe zao na hafla za maulid ya chuo hicho.
Katibu wa Madrasa ya Tauin Mwera Ndg Hamad Ali, akisoma dua baada ya kumalizika kwa hafla hiyo katika viwanja vya dunga zanzibar.

Chanzo: ZanziNews

No comments :

Post a Comment