Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, February 26, 2015

NO MORE GNU - says Waride Bakari Jabu!!

Katibu wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride Bakari JabuCCM zanzibar hatutaunda serikali ya GNU

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema hakitaunda tena Serikali ya Umoja wa Kitaifa baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kutokana na baadhi ya washiriki wake kuvuruga utaratibu na misingi ya kuanzishwa kwa serikali hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride Bakari Jabu wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini hapa jana.
Waride alisema makubaliano yanayotokana na kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa sasa yameanza kuvurugwa na kukiukwa kidogo kidogo katika misingi yake mikuu huku kauli za chuki na uhasama zikitawala.
Alikumbusha viongozi wa vyama vya siasa kwamba sababu za kuwapo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni tofauti za kisiasa na kauli za chuki ambazo zilisababisha kuwepo kwa malumbano ya kisiasa katika majukwaa ya kisiasa.
Alisema kwa bahati mbaya, misingi hiyo sasa imeanza kuyumba na kuporomoka kidogo huku matusi na kejeli kwa viongozi wakuu wa serikali akiwemo Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, zikichukua nafasi kubwa.
“Chama Cha Mapinduzi kimesikitishwa sana na kauli za chuki na uhasama, zinazotolewa na Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad ambazo zinaashiria kuyumba kwa serikali ya umoja wa kitaifa na kurudisha chuki na uhasama,” alisema.
Waride alifafanua kwamba CCM ambayo ni mshirika anayeunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa, inatamka bayana kwamba haipo tayari kushiriki kuunda serikali hiyo baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Alifahamisha CCM haikuwa na sababu ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa sababu ilipata ushindi wa kutosha, uliowafanya kuunda serikali. Hata hivyo ilifanya hivyo kwa ajili ya kukidhi matakwa ya sheria.
“CCM haioni sababu tena ya kuwepo kwa serikali ya umoja wa kitaifa kwa sababu wenzetu CUF wamekuwa wakitoa kauli za chuki na uhasama zinazorudisha nyuma matarajio ya wananchi wa kuwepo maridhiano ya kisiasa,” alisema.

No comments :

Post a Comment