Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, February 22, 2015

MCHAKATO KATIBA MPYA: Hamad: Kwa nini Wazanzibari wanapaswa kupitisha Katiba

Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed 
KWA UFUPI
  • Katiba Inayopendekezwa haina tatizo kubwa, hasa ikizingatiwa kuwa kuna maeneo mengi yenye migororo baina ya Wazanzibari na Watanganyika, yamefanyiwa kazi.
Wakati Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba ukifikia hatua ya Kura ya maoni inayotarajiwa kupigwa Aprili 30 mwaka huu, watu wameendelea kutoa maoni yao.
Wapo wanaoamini kwamba, mchakato huo hautapita kutokana na mambo kadhaa wanayoyaeleza na wengine wanaosema kuwa hawana shaka na kupitishwa kwa Katiba Inayopendekezwa katika kura ya maoni.
Mbunge wa Wawi (CUF), kisiwani Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed ni miongoni mwa watu wanaoamini kuwa Katiba Inayopendekezwa itapita. Anasema hana shaka Katiba hiyo itapita hata Zanzibar kutokana na maboresho mbalimbali yanayohusu kero za Muungano.
Anasema pamoja na kasoro nyingi zinazoelezwa, Katiba Inayopendekezwa haina tatizo kubwa, hasa ikizingatiwa kuwa kuna maeneo mengi yenye migororo baina ya Wazanzibari na Watanganyika, yamefanyiwa kazi.
“Lakini pamoja na yote hayo nishukuru kwa hatua iliyofikiwa. Ningeomba kwanza, vyombo vya habari vijaribu kueleza na upande wa mazuri yaliyopitishwa kwenye rasimu hiyo...Kwa mfano suala la mafuta ambalo lilishindikana kwa miaka mingi tangu enzi za Rais Hayati Karume, lakini limewezekana sasa kwa Rais Dk Shein,”  anaeleza.
Hamad anaeleza kuwa Katiba Inayopendekezwa imeingiza mambo mengi ya msingi ambayo yalikuwa kilio cha Wazanzibari, hivyo kustahili kupigiwa kura ya ndiyo, tofauti na madai ya wengi kwamba haifai.
“Katiba imeingiza mambo yote ya msingi yaliyokuwa yakipigiwa kelele na Wazanzibari. Wengine wanasema Katiba imevunjwa na Zanzibar, lakini siyo kweli ifahamike kwamba yapo mambo yanayounganisha kikatiba na mengine ni makubaliano,” anasema na kuongeza:
“Nitakupatia mfano, Cubeq waliingia kwenye kura ya maoni mara sita sasa tangu walipohitaji kujitoa Canada, lakini waliambulia asilimia 49, walipohojiwa tatizo nini? Wakasema tatizo ni uwakilishi basi wakapewa nafasi ya kuiwakilisha Canada kupitia Unesco je wamevunja Katiba?”
Anaendelea “Ni kama wanandoa, mambo mengi wanakubaliana ambayo ni kinyume na ndoa yao, je ndoa inakuwa imevunjika?”
Hamad anasema siyo kila kitu kinaweza kuingia kwenye Katiba na hata madai ya Wazanzibari yatamalizwa kwa hatua. Muungano ni damu siyo Katiba hebu angalia Watanganyika ambao ni asilimia 60 wanaoishi Zanzibar leo hii tukivunja Muungano tutawapeleka wapi?”
Kwa mujibu wa Hamad, Wazanzibari wanahitaji mikopo na misaada bila vikwazo na kama hivyo vikipatikana, kilichobaki na mambo ya utawala.
Anabainisha kwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba ulionekana kuvurugika kutokana na mgawanyiko uliojitokeza kwenye Bunge la Katiba, lakini katika uhalisia wake, hauna matatizo mengi.
“Makosa yaliyofanyika ni pamoja na kuruhusu vyama vya siasa kuingia na msimamo wake au sera yake juu ya aina ya muundo wa Serikali inaoutaka. Hilo ni kosa ambalo lilisababisha kuwa na mpasuko bungeni.”
Hamad anasema hoja ya vyama juu ya muundo wa Muungano ilitakiwa kuamuliwa na Watanzania wenyewe na siyo Bunge la Katiba.
 “Tume ya Jaji Joseph Warioba alipewa hadidu za rejea zilihitaji kusimamia msingi wa Muungano. Hata hivyo hadidu hiyo hazikutoa mwongozo wa aina gani ya Muungano unaohitajika.
Wanaoipinga
Kauli ya Hamad inapingana na msimamo wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), unaotaka mchakato huo usitishwe kwa kuwa sheria imevunjwa. Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba anasema pamoja na uzuri wake mchakato wa mabadiliko ya Katiba umevurugwa takriban katika hatua zote, ikiwamo Sheria ya Kura ya Maoni.
“Zaidi sana sheria yenyewe tayari imevunjwa. Kwanza haipatikani kiurahisi mitaani, lakini tayari Rais ameivunja kwa kutangaza tarehe ya kura ya maoni. Yeye (Rais) jukumu lake lilikuwa kutangaza ratiba ya mchakato  na siyo tarehe ya kura. Tarehe ya kura inatakiwa kutangazwa na Tume ya Uchaguzi kwa mujibu wa sheria,” anasema.
Kwa mujibu wa Profesa Lipumba kasoro nyingine ya Sheria ya Kura ya Maoni ni Katiba Inayopendekezwa kutowasilishwa kwenye Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na kuridhiwa, jambo ambalo pengine, linaweza kubatilisha mchakato mzima wa upigaji kura.
“Kwa kutowashirikisha, Wazanzibari wana haki ya kususia mchakato huo. Walipaswa kupelekewa Katiba Inayopendekezwa ili wairidhie kwenye Bunge lao lakini hili halikufanyika,” anasema. Anaendelea kueleza kuwa sheria hiyo pia inawanyima Wazanzibari haki kwa sababu imesema katika kifungu cha 34 kuwa Wazanzibari watahesabiwa Bara na Zanzibar. “Utawezaje kufanya hivyo wakati huna utaratibu wa kuwatambua Wazanzibari na Watanganyika kama siyo kutaka kuchakachua matokeo ya kura?” anahoji.
Kasoro nyingine ya Sheria ya Kura ya Maoni kwa mujibu wa Profesa Lipumba ni kutowapa wananchi fursa ya kuitambua Katiba Inayopendekezwa kwa kuwasambazia nakala na kutofanyika kwa zoezi la utoaji elimu kwa umma kwa wakati.
“Elimu kwa umma ilipaswa kuanza kutolewa mara baada ya Katiba Inayopendekezwa kuchapishwa kwenye gazeti la Serikali, lakini hilo halikufanyika,” anasema.
Madai ya Hamad
Hata hivyo, Hamad anasema kinachowasumbua wapinzani ni ndoto za kugawana madaraka katika Muundo wa Serikali tatu.
“Mimi naamini hata kama kuna kasoro, bado zinazungumzika hivyo sioni mantiki ya kushinikiza kura ya maoni.isipigwe kwa muda uliopangwa.”

No comments :

Post a Comment