Kaimu meneja mkuu wa tigo, Cecile Tiano akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaamlelo .Kulia ni Afisa Masoko wa kampuni hiyo George Wanyancha.Picha na Said Khamis
KWA UFUPI
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Meneja Mkuu wa mawasiliano Tigo, Cecile Tiano amesema kampuni hiyo imepanga kutumia kiasi hicho cha fedha kuimarisha kiwango bora cha huduma zake na inawapa watanzania fursa upatikanaji wa huduma yake mahali walipo.
Dar es salaam,Kampuni ya mawasilano ya Tigo inatarawajia kuwekeza Dola million 120 ambao ni sawa na Sh221bilioni ndani ya mwaka 2015 kwa kupanua wigo wa mtandao ikiwa ni pamoja na kuweka minara 787 mipya nchini
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Meneja Mkuu wa mawasiliano Tigo, Cecile Tiano amesema kampuni hiyo imepanga kutumia kiasi hicho cha fedha kuimarisha kiwango bora cha huduma zake na inawapa watanzania fursa upatikanaji wa huduma yake mahali walipo.
Amesema baadhi ya minara hiyo itakayokuwa na uwezo wa 3G na 4G itapelekwa Zaidi maeneo ya vijijini lengo likiwa ni kuwafikia watu walioko vijijini ili waweze kutumia huduma ya intaneti bila usumbufu wowote
“Minara hii ya 3G na 4G itaongeza upatikanaji wa huduma katika maeneo mengi ya vijijini, pia itaongeza upatikanaji wa intaneti: na kuongeza kuwa kwa sasa kuna Zaidi ya minara 20,000 nchi nzima.
Tiano amesema mwaka huu inataka kuongeza mara mbili ya maduka ya hudumu kwa wateja, kutoka maduka 42 mpaka kufikia 100, lengo likiwa ni kuhakikisha huduma ya tigo ipo karibu na wateja .
Pamoja na hayo Tiano Aliongeza kusema Tigo imebuni bidhaa na huduma mbalimbali kama facebook kwa Kiswahili ,Tigo pesa App,kwa watumiaji wa simu za Android na ios na ni Kampuni ya simu ya kwanza Afrika Mashariki kuanzia huduma ya kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu kimataifa ,yenye uwezo wa kubadili fedha za kigeni.
Alifafanua kuwa kwa sasa Tigo ina wateja zaidi ya million 7 na inatoa ajira za moja kwa moja na kwa namna ya mbalimbali kwa watanzania Zaidi ya 100,000 ambao wanajumuisha wafanyakazi wa huduma kwa wateja wa kutuma na kupokea fedha ,watu wa mauzo pamoja na wasamabazaji.
No comments :
Post a Comment