Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (pichani), alitoa agizo hilo jana baada ya kukabidhi vihori vya kubebea mwani kwa wakulima wa mwani wa Unguja na Pemba.
Dk. Shein alisema kuwa ni wajibu wa Serikali kuwaunga mkono wananchi kwa kuwajengea uwezo, ikiwemo kuwapatia masoko, mafunzo muhimu na fursa za mikopo pamoja na kuongeza kasi katika kutafuta masoko mapya.
Dk. Shein alisema kuwa dhamira ya Serikali ni kuona kuwa wakulima wa zao la mwani wanaongeza kiwango cha uzalishaji wa mwani na uwezo wao wa ubunifu katika kutumia rasilimali zilizoizunguka Zanzibar, ili wajikwamue kiuchumi na kufikia malengo la Mpango wa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupambana na Umasikini Zanzibar awamu ya pili (MKUZA II).
Aidha, Dk. Shein alieleza haja ya kutumia utaalamu uliotumika hadi bei ya karafuu ikaongezeka ili pia bei ya zao la mwani ikaongezeka huku akieleza kuwa Serikali itaendeleza jitihada zake za kuwaunga mkono wakulima wa mazao mbali mbali na kuhakikisha kuwa bei wanazolipwa kwa mazao yao inalingana na jitihada zao.
Dk. Shein alihimiza kuwapo kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH) kwa ajili ya kufanya utafiti juu ya njia bora za kuzalisha zao hilo ikiwa nji pamoja na kuwatafutia wakulima mbegu bora.
Pia, Dk. Shein aliwataka waliobahatika kupewa vihori hivyo kuvifanyia kazi ipasavyo na kuvitunza huku akiahidi Serikali kuendelea kutafuta njia zaidi za kuwasaidia wakulima wa mwani hapa nchini.
CHANZO: NIPASHE
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na mwakilishi wa VSO Tanzania Jean Van Wetter wakati alipowasili katika viwanja vya Ukimbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja leo katika hafla ya sherehe ya kukabidhi Vihori kwa wakulima wa Mwani
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Waziri wa Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana,Wanawake na Watoto Bi Zainab Omar Mohamed (wa pili kushoto) na Katibu wa Wizara hiyo Bi Asha Ali Abdalla (kulia)wakati alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja leo katika hafla ya sherehe ya kukabidhi Vihori kwa wakulima wa Mwani
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiangalia bidhaa, kwa Mjasiriamali Ndg Khamis Yussuf Machano,zilizotengenezwa kwa kutumia zao la mwani nakikundi cha Ulezi ni Kazi cha shehia ya Fujoni Jimbo la Kitope) wakati wa sherehe za kukabidhi Vihori kwa wakulima wa mwani hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa wananchi wakati sherehe za kukabidhi Vihori kwa wakulima wa mwani katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa wananchi wakati sherehe za kukabidhi Vihori kwa wakulima wa mwani katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja leo
Akinamama wakulima wa mwani kutoka sehemu tofauti za Unguja na Pemba wakiwa katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja katika sherehe za kukabidhi vihori kwa wakulima wa mwani kwa Mikoa ya Unguja na Pemba leo
Baadhi ya Viongozi,Wananchi na wakulima wa mwani wakiwa katika sherehe za kukabidhi vihori kwa wakulima wa mwani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja ambapo mgeni rasmi akiwaRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Kihori Bi.Zainab Daudi Haji mkulima wa mwani wa Uroa Wilya ya Kati Mkoa wa Kusini wakati wa sherehe za kukabidhi vihori kwa wakulima wa mwani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Kihori Bw.Kombo Salim Hamadi mkulima wa mwani wa Tumbe Magharibi Kaskazini Pemba wakati wa sherehe za kukabidhi vihori kwa wakulima wa mwani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
No comments :
Post a Comment