Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, March 10, 2015

BARAZA LA WAWAKILISHI LAANZA TENA!

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA YA SHUGHULI ZA MKUTANO WA KUMI NA TISA WA BARAZA LA NANE LA WAWAKILISHI UTAKAOANZA TAREHE 11 MACHI, 2015

Mkutano wa Kumi na Tisa wa Baraza la Wawakilishi la Nane la Zanzibar unatarajiwa kuanza kesho siku ya Jumatano tarehe 11 Machi, 2015, saa 3.00 kamili asubuhi.

Shughuli za mkutano huo zitakuwa kama ifuatavyo:-
1.      Maswali  na Majibu:
Maswali 77 yatajibiwa kwenye mkutano huu.
2.      Miswada ya Sheria:
Miswada Minne (4) ya Sheria itawasilishwa na kujadiliwa,
Miswada yenyewe ni:-
(i) Mswada wa Sheria ya Kuweka Masharti ya Usajili na Usimamizi wa Wathamini na Mambo Mengine Yanayohusiana na Hayo.
(ii) Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Kamisheni ya Ardhi na Mambo Mengine Yanayohusiana na Hayo.    
(iii) Mswada wa Sheria ya Kufuta Sheria ya Miradi ya Maridhiano Namba 1 ya 1999 na Kutunga Sheria Mpya kwa ajili ya Kuanzishwa na kuendesha mashirikiano baina ya Sekta ya Umma na Binafsi na Mambo Mengine Yanayohusiana na Hayo.
(iv) Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Baraza la Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar na Mambo Mengine Yahayohusiana na Hayo.

3. Kuwasilisha mbele ya Baraza, Sheria ya Kura ya Maoni Nam. 11 ya 2013 ya Jamhuri ya Muungano kwa Mujibu wa Kifungu 132(2) cha Katiba ya Zanzibar.

4.  Taarifa za Serikali (Mawaziri) kuhusu Utekelezaji wa Maagizo ya Kamati za Kudumu za Baraza la Wawakilishi Mwaka 2013 /2014.

5. Ripoti za Kamati za Kudumu za Baraza la Wawakilishi za Mwaka 2014/2015.

6.   Taarifa ya Kamati Teule ya Upotevu wa Nyaraka.

7. Hoja ya Mjumbe kuhusu Ucheleweshaji wa Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi.

(Yahya Khamis Hamad)
KATIBU
BARAZA LA WAWAKILISHI,

10 Machi, 2015.                                          ZANZIBAR.

No comments :

Post a Comment