Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, March 29, 2015

JK: Maaskofu walitoa matamko ya hasira

> Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Askofu Zacharia John(kulia) baada ya mkutano na viongozi wa kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam ,Wa tatu kushoto ni Sheikh wa Mkoa wa  Dar es Salaam ,Alhad Mussa Salum.Picha na Venance Nestory. 
  • Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana katika mkutano wa kamati ya amani ya Mkoa wa Dar es Salaam iliyoshirikisha wajumbe kutoka mikoa mbalimbali nchini unaowajumuisha viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo akilenga kuzungumzia tamko hilo la TCF walilolitoa Machi 12, mwaka huu.
Dar/Tanga/Arusha. Wakati Rais Jakaya Kikwete akisema msimamo wa Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF) wa kuwataka waumini wao kuipigia kura ya hapana Katiba Inayopendekezwa ni wa hasira pia usiokuwa na tija kwa maendeleo ya Taifa, baadhi ya maaskofu wameshikilia msimamo huo.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana katika mkutano wa kamati ya amani ya Mkoa wa Dar es Salaam iliyoshirikisha wajumbe kutoka mikoa mbalimbali nchini unaowajumuisha viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo akilenga kuzungumzia tamko hilo la TCF walilolitoa Machi 12, mwaka huu.
Katika tamko hilo lililosainiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dk Alex Malasusa, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa na mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania (CPCT), Askofu Daniel Awet liliwataka waumini wake kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapigakura na kuipigia kura ya hapana Katiba hiyo.
Jukwaa hilo lilitaja sababu mbili za uamuzi wake huo kuwa ni Muswada wa Mahakama ya Kadhi kukiuka misingi ya Taifa kuwa na Serikali isiyo na dini na Kura ya Maoni kusababisha mgawanyiko.
“Hivyo basi, Jukwaa linawataka waumini wake wote wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, waisome Katiba Inayopendekezwa na kushiriki kikamilifu vipindi vya elimu juu ya Katiba Inayopendekezwa na kisha wajitokeze kwa wingi kupiga kura ya hapana,” lilisema tamko hilo.
Katika hotuba yake iliyodumu kwa saa 1.16, Rais Kikwete alianza kwa kuwaomba radhi viongozi hao kwa kuchelewa kwa akisema alikuwa na majukumu mengi. Mkutano huo ulikuwa uanze saa 3.00 asubuhi lakini Rais Kikwete alifika saa 6.30 mchana.
Alisema “Taifa linapitia hali isiyokuwa ya kawaida, tusipokuwa makini kuidhibiti itakuwa ni tatizo, ni kazi kubwa inayohitaji moyo, uvumilivu na viongozi wenye kujali masilahi ya Taifa.”
“Mwelekeo wa mambo hauhitaji uwe bingwa kujua hali hairidhishi sana na kama hatutachukua hatua hatuwezi kufika na tutasababisha uvunjifu wa amani za kidini na moto wake ni mkali sana,” aliongeza Rais Kikwete aliyekuwa akizungumza kwa umakini na taratibu.
Jukwaa la wakristo
Kuhusu tamko la Jukwaa la Wakristo, Rais Kikwete alisema wakati Taifa likisubiri kuona mchakato wa Katiba unakwenda hatua za mwisho kumekuwapo na matamko kadhaa ambayo hayakumfurahisha.
“Nimeyasoma matamko hayo yote kwa umakini, imenishangaza, imenisikitisha na kunihuzunisha. Siamini kwa nini wamefikia huko kwa kuunga au kutokuunga mkono,” alisema Rais Kikwete aliyekuwa akizungumza kwa sauti ya chini wakati wote wa hotuba yake.
“Kinachonisumbua ni kuipa sura na mtazamo wa kidini Katiba Inayopendekezwa, kama ingekuwa inakinzana na uhuru wa kuabudu hapo ingekuwa sawa lakini ibara ya 41 inatambua uhuru wa kuabudu na kuitangaza dini, sasa katika mazingira hayo kuwaeleza waumini kuikataa inanipa tabu sana,” aliongeza.
Alisema, “Katiba hii imezingatia na kutambua makundi mbalimbali na mimi sina haya kuwaeleza kuwa tuipitishe kwani licha ya upungufu ilionao, haifikii hii ya sasa. Tusipoipitisha tutaendelea kuitumia hii na sidhani kama kuna Rais atakuja na kuanza na mchakato wa Katiba, hivyo hii hii tuipitisheni kama ina upungufu utafanyiwa maboresho kwani Katiba siyo Msahafu au Biblia.”
Rais Kikwete anayemaliza muda wake wa uongozi mwaka huu alisema: “Waacheni waumini waamue Katiba wanayoitaka wao, hayo matamko niliyoyasoma yamejaa hasira kwa Serikali kupeleka bungeni Muswada wa Mahakama ya Kadhi.”
Katika kujenga hoja hiyo alisema Serikali imepeleka muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali ambao ndani kuna kifungu kinachohusu Mahakama ya Kadhi, jambo ambalo siyo geni kwa kuwa limekuwapo kwa kipindi kirefu.
“Tunachotaka kufanya ni kutambua hiki ambacho Waislamu wamekianzisha kwa kuwa na Mahakama ya Kadhi na makadhi, Serikali haitawasimamia wala kuziendesha mahakama hizo, hivyo hazina tatizo lolote,” alisema Rais Kikwete akitanguliza maneno kwamba, “naomba nitumie lugha ambazo sitowakwaza watu.”
“Siyo kila anachokitaka mtu kitakuwamo katika Katiba, mfano mimi na CCM tulikuwa na mambo 60 tuliyoyaona ya msingi sana yawemo katika Katiba lakini sidhani kama yanafika hata 12...kwa kuwa mchakato unaendeshwa kisheria basi tuuache umalizike kisheria,” aliongeza.
“Sidhani mnachokifanya ni sawasawa, mnawakwaza waumini wenu, waacheni waamue wao wenyewe kwani mkiendelea hivyo watawaona ninyi hamfai kwani kila mtu katika hili ana msimamo wake, mwingine anaona hili linafaa mwingine anaona halifai.”
Awali, Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum ambaye pia ni Sheikh wa mkoa huo, alisema wameamua kumwalika Rais Kikwete kuzungumzia na viongozi hao kutokana na Taifa kuwa katika hali ya sintofahamu.
“Tumeamua kukualika wewe uzungumze na viongozi wa dini zote zitakazosaidia kubadilisha hali iliyopo sasa. Umevumilia mengi kama Watanzania walikuudhi na kukukera kwa niaba yao uwasamehe,” alisema Sheikh Salum.
Naye Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Askofu Valentino Mokiwa alisema baada ya mkutano huo kuwa kuna umuhimu wa kutafakari mambo yanayosumbua na kuendelea kusumbua sana.
“Bado sijajua kama hotuba yake (Rais) aliyoitoa itatoa dira ya mchakato huu wa Katiba, tusubiri kuona kipi wananchi wataamua,” alisema Askofu Mokiwa ambaye pia ni Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Dar es Salaam.
Umoja wa makanisa Tanga
Katika tamko lake Umoja wa Makanisa Mkoa wa Tanga pamoja na kuwataka Watanzania kuikataa Katiba Inayopendekezwa, umeishauri Serikali kusogeza mbele Kura ya Maoni.
Msimamo huo ulitangazwa na Mwenyekiti wa umoja huo, Askofu Dk Jotham Mwakimage aliyezungumza na waandishi wa habari baada kikao cha maaskofu na wachungaji wa makanisa mbalimbali ya Tanga.
Alisema kikao chao kilichofanyika wiki iliyopita katika Kanisa la Agape jijini Tanga na kuhitimishwa jana, kimeamua kutambua na kuheshimu tamko la Jukwaa la Wakristo lililotolewa Machi 10, mwaka huu la kuwaomba Watanzania waipigie kura ya ‘Hapana’ Katiba Inayopendekezwa.
Sababu za kuikataa
Alisema Katiba hiyo ni imeligawa Taifa la Tanzania, iliandaliwa na kupitishwa kwa hila na kimabavu na ndiyo sababu inalazimishwa ipigiwe kura ya ‘Ndiyo’ bila kuruhusu masahihisho ya makosa yaliyomo.
Sababu nyingine kwa mujibu wa tamko hilo ni kwamba Katiba Inayopendekezwa iliandaliwa kwa hila ikiwa na madhumuni ya kuondoa Rasimu ya Katiba iliyotokana na mawazo ya wananchi walio wengi yaliyokusanywa na kuratibiwa na Tume ya Jaji Warioba.
“Walioleta msukumo wa kupitisha Katiba kimabavu, ndiyo wanaochochea uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi ili kuigawa nchi kidini,” alisema Mwakimage wakati akielezea sababu ya nne ya kutounga mkono katiba pendekezwa.
Umoja huo wa makanisha umesema katika tamko hilo kwamba ili kuondoa mkanganyiko, unaishauri Serikali kusogeza mbele Kura ya Maoni kwa sababu muda wa mwezi mmoja hautoshi kwa wananchi kuisoma, pia nakala zilizotolewa ni chache.
Sababu nyingine ya kupendekeza kusogezwa mbele kwa Kura ya Maoni ni kutoa nafasi ya kutosha ya kuboresha Daftari la Wapigakura na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
“Sisi umoja wa makanisa tunasisitiza kuwa Watanzania wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la Wapigakura na kupigia Katiba Inayopendekezwa kura ya Hapana, sawa na tamko la maaskofu,” alisema Mwakimage.
Baraza la makanisa
Wakati huohuo, Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT) limetoa tamko kuhusu hali ya kisiasa nchini likiwamo suala la Katiba Inayopendekezwa,
Mahakama ya Kadhi na kusisitiza uamuzi wa kuwataka Wakristo kujiandikisha kwa wingi na kuipigia kura ya ‘Hapana’ katiba hiyo.
Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu CPCT, Askofu David Batenzi alitoa tamko hilo jana katika Kanisa la Bethel jijini Arusha mbele ya maaskofu wakuu 70 waliohudhuria na kujadili pamoja na mambo mengine, hali ya kisiasa nchini, akisema wamefikia hatua ya kutoa tamko hilo ili kuondoa mkanganyiko uliokuwapo.
Akifafanua mkanganyiko huo, Askofu Batenzi alisema kumekuwapo madai ambayo siyo ya kweli kuwa miongoni mwao kuna maaskofu wanaonyesha nia ya kuwaunga mkono wagombea urais na wengine wanatoa matamko kinzani dhidi ya tamko la Jukwaa la Wakristo (TCF), chombo ambacho CPCT ni mwanachama.
Askofu Batenzi alisema kuwa CPCT haina chama wala mgombea na kwamba wanaamini katika kumwomba Mungu awape kiongozi atakayelifaa Taifa.
“Mtu yeyote anayedai kuwa ni Mpentekoste aliyetenda au atakayetenda kinyume na msimamo huu, hakutumwa na wala hatakuwa ametumwa na CPCT,” alisema.
Alisema uwakilishi wa viongozi na wajumbe wa CPCT kwenye kikao cha TCF kilichotoa tamko, ulikuwa na baraka zote za baraza hilo na madai yoyote kwamba CPCT inaburuzwa na mwenyekiti na katibu wake kwenye tamko hilo yapuuzwe, kwa kuwa hayana msingi wowote.
  • Mh.Rais alitatikiwa angekutana na viongozi wote wale wliotoa tamko na sio hao ambao waaumini wanawaona kama wao wako upande wa serikali.swala la mahakama ya kadhi haliitaji mjadala lazima serikali ikae mbali nalo.NCHI hii haina dini wala serikali yake haina dini,iweje leo serikali inaamua kusimamia na kuiratibu swala hili.mimi nadhani KATIBA itamke kuwa mgombea atakaye toa ahadi zenye mirengo ya dini aondolewe kwa kuwa hafai.
    • Avatar
      Muumini atakaye piga kura ya ndiyo ana dhambi za kutubu,hii si katiba tuliopendekeza wananchi, Bali ni katiba ya wakina Makonda,
        • Avatar
          KIKWETE LIKES THIS KIND OF RELIGIOUS LEADERS,THE SUBMISSIVE ONES WHO CAN JUST NOD THEIR HEADS TO EVERY INSENSIBLE ISSUE THE GOVERMENT MAY BRING TO THEM.
            • Avatar
              Mimi ambacho sielewi, ni kwa nini serikali inataka kuingiza mahakama ya kazi kwenye katiba na sheria za nchi. Ni mapungufu gani yaliyomo katika sheria za ndoa na mirasi za serikali za sasa, ambazo zinawanyima haki waislamu mpaka watafute haki hiyo kwenye mahakama ya kazi. Na kama zipo kwa nini serikali isihiboreshe sheria hiyo hili kutoa haki sawa kwa watu wote bira kuleta mahakama ya kazi. Unajua mahakama ya kazi haitumiki hata kwenye nchi za kiislam kama Saudi Arabia na misri, sasa yeye anasema wakristo wanalipa swala hili umbo la kidini. Lkn ni serikali ndio inaanza kuleta dini ndani ya sheria za nchi. Mahakama ya kadhi ni mahakama ya kidini. swala hili sio la kuletwa na serikali bungeni. wangeachiwa waislamu wenyewe wanaotaka kuhukuniwa nayo wakifa waandike kwenye barua zao za wosia na kuziacha kwa wanasheria wao. Familia zao zitafuata huo wosia.
                • Avatar
                  ndugu yangu nyaga nadhani haufahamu historia ya sharia za nchi hii vizuri kwa maana ni sheria za kadhi zilikuwepo Tangu kipindi cha ukoloni na kipindi cha uhuru nyerere aliziondoa mwaka 1977. Saudi Arabia wanaongozwa na sharia hivyo hakuna haja ya kuwa na mahakama ya kadhi..misri wanazo fanya reseach vizuri.....sharia ya dini ya kiislam imetoa muongozo kwenye sekta zote za maisha ya mwanadamu ya nini kifanyike kunapotokea kitu Fulani au tatizo hivyo sheria za serikali hazina muongozo huo kwanza serikali haina sheria inayohusu mirathi kama haufahamu.....na pia mbona kuna balozi wa papa hapa nchini ambaye serikali inamtambua hali ya kuwa Vatican sio nchi?....sasa mimi kama muislam nitaipigia kura katiba pendekezwa endapo kuna suala la mahakama ya kadhi...na nyie wakristo kama hamtapig sisi tutapiga sasa nyie pigeni ya hapana na sisi tutapiga ya ndio...walio wengi watashinda.
                    • Avatar
                      AJENDA HII ILILETWA NA WANASIASA MUFLISI WANAOFANYA SIASA ZA BEI RAHISI WAKIONGOZWA NA KIKWETE.HIVI KAMA WAKATOLIKI WANAWEZA KUSIMAMIA SHERIA ZAO ZA KANISA BILA KUINGILIWA NA SERIKALI KWA NINI WAISLAMU TUTEGEMEE MGONGO WA SERIKALI?KAMA TUNATAKA KUJENGA HESHIMA YETU TUSITEGEMEE SERIKALI BALI NI WAUMINI WENYEWE TUNATAKIWA KUISIMAMISHA DINI YETU WENYEWE.NITAIPINGA MAHAKAMA HII KWA NGUVU ZOTE KAMA ITAKUWA AJENDA NA ILANI YA UCHAGUZI NA KUIDHALILISHA IMANI YETU BADALA YA KUWA CHOMBO CHA KUSIMAMIA HAKI KWA WAISLAMU BILA KUJALI NI CCM AU UKAWA.
                      • Avatar
                        HAYAKUWA MATAMKO YA HASIRA MR.PRESIDENT NI YA UKWELI MTUPU NA TUSIDANGANYANE.KAMA WEWE UNATAKA KUWA MKWELI ONDOA MAHAKAMA YA KADHI KWENYE BUNGE NA SIVINGINEVYO.HILI SWALA LIKIENDELEA NI WEWE UMELIPA NAFASI KATIKA UONGOZI WAKO.
                          • Avatar
                            mchakato wa mahakama ya kadhi uko pale pale mtake mistake utafayika tu sisi waislam tutaipigia kura katiba pendekezwa...kam biblia haijatoa muongozo wa kuhusu maisha yenu na nini mfanye msimlaumu mungu...kuweni wapole wacha maisha yaendelee sisi waislam tutaipigia katiba hata bila ya nyinyi
                              • Avatar
                                kabula hujabisha na kuikataa mahakama ya kadhi uliza upewe ufafanuzi kuhsu mipaka yake na mambo inayoenda kushugulikia, sisi lengo letu ni kutambuliwa kisheria ili maamuzi itakayokuwa inafanya yatekelezwe na muumini kw kufuata mwongozo wa quran na suna baada ya kukubali na kujitambua kwamba yy ni muislam na siyo kukimbilia mahakama kw kufuata hukumu ambayo sio katka quran na suna. na mambo inayoenda kushughulikia yameanishwa. na siyo hukumu zote zilizokatka quran maana katiba yetu aindeshwi kw misingi ya dini yyoto muondoe wasiwasi, nasi mtupe uhuru wa kuabudu kama katiba inavyosema kla mtu anahuru wa kuabudu na hiyo mahakama ya kadhi ukihukumiwa nayo yale yaliyoainishwa ni moja wapo ya ibada. jamani msutunyanyase kama vile ss syo watanzania ambao tunaieshimu katiba uhuru wa kuabudu.

                          No comments :

                          Post a Comment