- Akiwasilisha ripoti ya Kamati Teule ya kuchunguza upotevu wa nyaraka za serikali katika Baraza la Wawakilishi, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mahamoud Mohammed Mussa alisema tukio la wizi huo lilianza kujulikana kuanza Julai mwaka 2013 na Baraza kulazimika kuunda kamati ya uchunguzi.
Zanzibar. Nyaraka nyeti za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zilizokuwa zimehifadhiwa katika Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu za Taifa, zimeibwa na mmoja wa watuhumiwa ni ofisa mwandamizi wa Ubalozi mdogo wa Omani uliopo Zanzibar.
Akiwasilisha ripoti ya Kamati Teule ya kuchunguza upotevu wa nyaraka za serikali katika Baraza la Wawakilishi, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mahamoud Mohammed Mussa alisema tukio la wizi huo lilianza kujulikana kuanza Julai mwaka 2013 na Baraza kulazimika kuunda kamati ya uchunguzi.
Mahamoud alisema nyaraka hizo zilikuwa zimehifadhiwa katika chumba maalumu na kuhifadhiwa katika masanduki lakini watu walifanikiwa kula njama za kuiiba nyaraka hizo kwa kuwatumia baadhi ya wafanyakzi wa Taasisi hiyo.
Aliwambi Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wezi hao walitumia mbinu mbalimbali ikiwemo ushawishi wa fedha na zawadi za vyakula zikiwemo tende wakati mpango wa kuibiwa nyaraka hizo ukiendelea kufanyika kwa siri kubwa kabla ya kufanikiwa.
Mahamoud alisema miongoni mwa nyaraka zilizoibiwa ni pamoja na nyaraka za kumbukumbu za Utawala wa Sultani Sayydid barghash Bin Said kabla ya Mapinduzi na waraka uliyotumika kupinga marufuku biashara ya Utumwa kufanyika Zanzibar mwaka 1873 pamoja na kumbukumbu za ujio wa wamisionari Zanzibar ambao walifanya kazi ya kueneza ukiristo Afrika Mashariki.
Hata hivyo alisema kwamba baadaya Kamati kufanya uchunguzi umegundua mpango wa wizi wa nyaraka hizo umeratibiwa na Ofisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Omani Humoud Abdalla AL Rashid na hatua za kumkamta na kumfugulia mashitaka zimekwama kutokana na kuwa na kinga ya kutoshitakiwa ya Kidiplomasia.
Alisema kwamba Humoud kabla ya kufanikisha wizi wa nyaraka hizo alikwa akienda kila mara akiwa na vizawadi vya vyakula na kujenga uhusiano mkubwa na watendaji wa Taasisi hiyo kwa madhumuni ya kuendeleza hifadhi za kumbukumbu visiwani humo.
Aidha alisema pamoja ofisa huyo wa ubalozi kufungulikiwa kesi katika Kituo cha Polisi Mazizini Jeshi la Polisi limekwama kumkamata kutokan na mkataba wa Vienna.
wa kidiplomasia wa mwaka 1961 na sheria namba tano ya kinga na fursa 1986 kuweka kinga ya wanadiplomasia kukamatwa na kufunguliwa mashitaka.
Mohamoud alisema kwamba Uchunguzi pia umegunduwa Waziri mwenye na Kazi na Utawala Haroun ali Suleiman amelidaganya Baraza la Wawakilishi (BLW) kutokana na kauli yake aliyotoa kuwa Humoud hakuwa ofisa mwanadamizi wa ubalozi bali alikuja Zanzibar kama mfanyakazi kufanikisha shughuli za ukarabati wa Jengo moja la historia visiwani humo.
Alisema kitendo cha Waziri kinakwenda kinyume na mashariti ya kanuni ya 59 (3) ya kanuni za kudumu za Baraza la Wawakilishi ambazo zinakataza mjumbe yeyote kutoa maelezo yasiyokuwa sahihi ya kubuni au kubahatisha katika chombo cha kutunga sheria.
No comments :
Post a Comment