Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, March 31, 2015

Marafiki wa Lowassa waja na staili mpya

Image result for lowassa

Moshi. Mbunge wa Moshi Vijijini na Mjumbe wa Nec ya CCM, Dk Cyrill Chami, amewaomba walimu zaidi ya 2,700 wamuombee Waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ili ‘ndoto’ yake iweze kutimia.
Wakati Dk. Chami akiwaomba walimu hao, mtandao wa marafiki wa Lowassa Kanda ya Kaskazini, juzi walikuja na staili mpya ya kumshawishi Mbunge huyo wa Monduli agombee nafasi ya Urais.
Staili hiyo mpya imekuja wakati CCM ikiwa imempiga ‘stopu’ kuendelea na utaratibu wake wa kupokea makundi ya watu wanaomshawishi kugombea urais na yeye (Lowassa)  kuridhia na kuwaomba wananchi wasubiri maelekezo ya CCM.
Marafiki hao ambao ni wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Kilimanjaro, walikwenda kitengo cha damu salama Kanda ya Kaskazini kuchangia damu kama njia ya kutambua na kuenzi upendo wa Lowassa.
Tukio hilo la wanafunzi hao kwenda katika kitengo hicho, kilitanguliwa na tukio la mkutano mkuu wa Chama cha Akiba na Mikopo (Saccos) ya Walimu Moshi Vijijini kufanya mkutano wao mkuu. Katika mkutano huo, Dk Chami aliyekuwa mgeni rasmi, aliwaambia amekwenda pale akiwa na salamu kutoka kwa Lowassa kwamba anawapenda sana walimu. “Anasema anawapenda na anawakumbuka sana na anawaomba mmuombee ili ndoto yake na ile safari yake (bila kuitaja) itimie,” alisema Dk Chami na walimu hao kulipuka kwa vigelegele.
Katika tukio la uchangiaji wa damu, wanafunzi zaidi ya 100 wa vyuo vikuu mkoani Kilimanjaro, walitumia tukio hilo kumuunga mkono Lowassa wakimsihi atangaze nia ya kuwania Urais 2015.
Mratibu wa marafiki wa Lowassa, Noel Nnko, alisema wanafunzi hao wameamua kuchangia damu kumuunga mkono kada huyo kwa vile wao hawana uwezo wa kutoa fedha za kuchangia fomu.

No comments :

Post a Comment