zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, March 20, 2015

TANZANIA INAMALIZWA NA RUSHWA!!!

hii kubeba wajawazito mgongoni ni fedheha kubwa.

20th March 2015

Habari kwamba wajawazito wanabebwa mgongoni wakati wa kupelekwa kituo cha afya Mgeta kujifungua kutokana na ubovu wa barabara katika kijiji cha Bunduki wilayani Mvomero, ni za kukatisha tamaa na ni janga kubwa kwa wanawake na vichanga. 
Habari ambazo zilipatikana kijijini hapo na kuandikwa na gazeti hili katika toleo lake jana ukurasa wa 21, zinasema kwamba hali hiyo inawakumba wakazi wa kijiji hicho kutokana na barabara yao kutokarabatiwa kwa miaka 20 sasa.
Uongozi wa kijiji hicho ulisema mipango ya kukarabati barabara hiyo imekwama kwa muda mrefu kutokana na fedha zinazotolewa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kutokukidhi gharama husika na kibaya zaidi hata zinazotolewa ni kidogo sana.
Wajawazito wanaobebwa na wale wanaoshindwa kutembea kufuata huduma ya afya baada ya kushindwa kujifunguliwa kwenye zahanati ya kijiji hicho, hivyo kulazimika kubebwa umbali wa kilometa 12 ilipo zahanati ya Mgeta.
Hali hii ipo katika maeneo mengi ya nchi hii, hasa yeye mwiinuko mkali. Ingawa kumekuwa na juhudi za kujenga zahanati kila kijiji kwa nia ya kusogeza huduma za afya karibu zaidi na wananchi, ubovu wa barabara, kutopatikana kwa dawa na vifaa tiba pamoja na uhaba wa wahudumu wa afya, imekuwa ni moja ya changamoto kubwa zinazokabili sekta ya afya nchini hivyo kuathiri ustawi wa jamii kwa ujumla wake.
Ingawa kiliometa 12 siyo umbali mrefu sana kwa kutumia usafiri wa ama baiskeli, bodaboda au gari, inapokuwa hakuna barabara ya kupitika, hali inakuwa mbaya zaidi kwani hata kama huduma zipo inakuwa vigumu kuzifikia.
Katika miaka ya hivi karibuni taifa hili limeshuhudia ujenzi wa barabara nyingi za lami, nia ikiwa ni kuunganisha miji mikuu yote ya mikoa kwa barabara hizo. Kwa hakika kazi kubwa imefanyika na inatia moyo kwamba maeneo mengi ya nchi sasa yamefunguka na yanafikika kwa urahisi kwa sababu ya kuimarika kwa miundombinu. Tunatoa pongezi kwa kazi hii iliyotukuka pamoja na kwamba kuna changamoto nyingi juu ya ubora wa baadhi ya barabara hizi.
Hata hivyo, pamoja na kazi hii nzuri ya kuunganisha miji mikuu yote ya mikoa kwa barabara za lami, kazi ni mbichi kabisa kwenye barabara za halmashauri, ndiyo maana wakazi wa kijiji cha Bunduki wilayani Mvomero, wanakabiliwa na adha ya kubeba wajawazito mgongoni ili kuwapeleka kituo cha afya umbali wa km 12.
Mbali na kitendo hicho kuhatarisha maisha ya wajawazito hao na watoto wanaotarajia kujifungua, pia kinaonyesha jinsi jamii yetu ilivyo nyuma kwa maana ya ubora wa huduma za kijamii. Pia ni aina nyingine ya udhalilishaji.
Tunajua kwamba wananchi wanalipa kodi ili wapate huduma kutoka serikalini. Huduma hizi ni pamoja na ujenzi wa miundombinu kama barabara kuu na zile za vijijini kama hii ya kijiji cha Bunduki.
Tunatambua kwamba uwezo wa serikali ni mdogo kutokana na majukumu mengi yaliyoko mbele yake, lakini pia tunajua kwamba kama msisitizo wa vipumbele ukitiliwa maanani, hata hicho kidogo kinachopatikana kinaweza kufanya kazi kubwa zaidi na hivyo kuepusha jamii na adha kama hii ya kuwabeba wajawazito mgongoni.
Kadhalika, kijiji ambacho kwa miaka 20 barabara yake haijakarabatiwa nacho kina walakini kwa maana ya kukosa kabisa maono ya kuhamasisha nguvu kazi ndani yao ili kufanya lolote kwenye barabara yao.
Hapa nchini vipo vijiji vingi mazingira ya kijiografia yake ni ya miinuko mikali sana, mvua zikinyesha barabara zao zinaharibika sana, lakini wamekuwa na mkakati wa kudumu wa kuzifanyia matengenezo kwa kutumia nguvu kazi yao wenyewe.
Tungependa kuchukua fursa hii kuutaka uongozi wa kijiji cha Bunduki kutambua kuwa kuongoza ni kuonyesha njia, kama fedha kwenye halmashauri kwa miaka 20 hazijapatikana, wataendelea kukaa hivyo mpaka lini? Ni vema sasa wakakaa kitako kwenye mkutano wa kijiji na kukubaliana ni kwa jinsi gani wanaweza kutumia nguvu zao wenyewe na rasilimali zao kujikwamua kwenye adha hii. 
Hatua za namna hiyo zinaweza kuwa ni za muda wakati wakisubiri halmashauri na hata serikali kuu kupata nguvu ya kuelekeza fedha kwenye barabara hiyo. Hakuna linaloshindikana kama nia ipo. Tujikumbushe kuwa kujitawala ni kujitegemea na kuongoza ni kuonyesha njia ya kutatua changamoto zinazokabili jamii. Kukaa na kulalamika pekee hakutoshi, tujaribu mbinu mbadala katika kukabiliana na changamoto za maisha.
CHANZO: NIPASHE

Wajawazito wajifungua kwa mwanga wa simu

15th August 2014

Wajawazito wa kata ya Mbuyuni ya halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, wanalazimika kujifungua watoto kwa kutumia mwanga wa tochi wa simu kutokana na zahati yao kukosa umeme.

 Diwani wa kata hiyo, Ally Kila, akichangia muktasari wa kamati ya kudumu ya elimu afya na, maji kwenye kikao cha baraza la madiwani la halmashauri hiyo, alisema kuwa maisha ya wajawazito hao yako hatarini endapo jitahada za kuipatia umeme zahanati hiyo hazitafanikiwa.

Alisema  zahanati hiyo ilikuwa na umeme wa wa  nishati ya jua,  lakini baadae paneli inayotumika kufua umeme huo iliibiwa  tangu mwaka 2012.

Alisema tangu wakati huo, zahanati hiyo haina umeme na kusababisha wajawazito hao kulazimika kutumia mwanga wa tochi ya simu wakati wakijifungua.

Diwani huyo alisema hali hiyo inawafanya wahudumu wa zahanati hiyo kufanya kazi katika mazingira magumu.

“Ni hali ya kusikitisha kuona akinamama wakijifungulia gizani ama kwakutumia mwanga wa tochi wa simu,” alilalamika.

Akizungumza katika kikao hicho, Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya hiyo, Jarry Khanga,  alisema kuwa zahanati hiyo imewekwa katika mpango wa kupatiwa huduma ya nishati ya umeme mwaka huu wa fedha wa 2014/15.

Alisema hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu, zanahati hiyo itakuwan imepata huduma ya umeme na kuwaondolea adha wananchi wanaoitumia kwa matibabu.

CHANZO: NIPASHE

Wajawazito wajifungulia mwanga wa simu

30th March 2014

Ukosefu wa umeme kwenye kituo cha afya  cha Ikonongo mkoani Shinyanga, umesababisha wajawazito kujifungua kwa msaada wa mwanga wa simu, hivyo kuongeza hatari ya vifo vya wazazi na watoto kutokana na huduma duni.

Wakizungumza na wanahabari mwishoni mwa wiki wilaya ya Shinyanga Vijijini, baadhi ya wanawake wa kata ya Salawe kilipo kituo hicho walisema hakina huduma muhimu kuanzia  vifaa vya uchunguzi wa maradhi,  maji kwenye wodi ya wazazi na miundombinu muhimu ya tiba.

Walisema kutokana na ukosefu wa nishati hiyo ya umeme wajawazito hasa  wanaojifungua usiku wanategemea mwanga wa taa za chemli kama kuna mafuta ya taa, mishumaa pamoja na mianga ya tochi za simu ambayo inatoa mwanga zaidi.

Chausiku Kashindye mmoja wa wanawake hao  alisema licha ya changamoto hiyo ya nishati vilevile kituo hicho hakina maji safi na salama ambapo wanawake  wanahitaji  baada ya kujifungua.

Alisema wazazi hao  hulazimika kwenda kuchota maji visimani, madimbwini, malamboni na mabwawa ambayo si salama kiafya hasa kwa wazazi na watoto hao walio  kwenye hatari ya kuambukizwa maradhi.

Naye Mganga mkuu wa kituo hicho Dk Simon Wilson, akizungumzia changamoto  hizo alipinga madai ya wajawazito kujifugua kwa mwanga wa  simu na kusisitiza kuwa wanatumia taa za kawaida.

Alisema wanatumia umeme wa mwanga wa jua na kwamba taa zake zinawashwa kuanzia saa moja jioni na kuzimwa saa tano usiku kutokana na kutokuwa na nguvu ya kutosha
Kwa upande wa Mwenyekiti wa kijiji cha  Azimio kilipo kituo hicho,  Twiga  Mashimba  alisema  kituo hicho kinahudumia  vijiji zaidi ya vitano  na kata tatu  ambazo ni Mwakitolyo, mwenge ,Salawe na kinakabiliwa pia na uhaba wa wodi ya watoto na kulazimika kuchanganya watu wazima na watoto.

“Kituo hiki cha afya kinahudumia zaidi ya watu 21,000 na kwa upande wa nishati ya umeme kulikuwa na sola mbili ambazo zilikuwa zinasaidia kuzalisha umeme wa kutosha lakini sola moja iliibiwa hivyo  kusababisha kituo chetu kukosa umeme wa kutosha”alisema Mashimba .
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment