Najua uchaguzi wa kura za maoni umemalizika, wana-CCM yafaa sasa tuwe pamoja.
Kitendo hicho kimemfanya Mwenyekiti wa kata ya Mahoje, Gekura Gisiri, kujivua uongozi kwa madai ya kupinga uteuzi wa mgombea udiwani katika kata hiyo.
Mmoja wa makada hao, Yusuph Mchika, alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na makada hao 50 wa CCM waliojitokeza kwenye mkutano huo Majohe jijini Dar es Salaam juzi.
Mchika alisema amefurahishwa na uamuzi wa Mwenyekiti wao kujizulu ili kuwaunga mkono kutokana na ubabaishaji ulijitokeza kwenye kura za maoni.
Gisiri alisema uongozi umejitahidi kutoa ushauri kwa viongozi wa juu wa Chama, lakini ameshangazwa kupitishwa kwa jina la mgombea huyo.
“Siwezi kumnadi mgombea ambaye kwa miaka mitano akiwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, hakufanya chochote, hivyo atakuwa mzigo kwangu kumnadi,” alisema.
Hata hivyo, mgombea udiwani huyo aliyeshinda kura za maoni, Kingalu akijibu madai hayo alisema kabla ya kuwania nafasi hiyo, alikuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mahoje na kufanya kazi nyingi ikiwamo kupambana na wimbi la wavamizi wa mashamba pori.
Hata hivyo, mgombea udiwani huyo aliyeshinda kura za maoni, Kingalu akijibu madai hayo alisema kabla ya kuwania nafasi hiyo, alikuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mahoje na kufanya kazi nyingi ikiwamo kupambana na wimbi la wavamizi wa mashamba pori.
“Najua uchaguzi wa kura za maoni umemalizika, ni vema wana-CCM tukarudi na kukaa pamoja ili kuondoa tofauti zetu. Mimi Kingalu nilipata kura 1,593 na Wilfred Batakanwa, alipata kura 896,” alisema.
Naye kwa upande wake, mgombea ambaye kuira za maon i hazikutosha, Batakanwa alisema ameshangazwa pingamizi zao kuwekwa kapuni na kupitishwa Kingalu kuwa mgombea udiwani kata ya Majohe.
“Uamuzi umetolewa na kamati ya uteuzi, tunapaswa kusubiri maamuzi ya nguvu ya umma Oktoba 25, mwaka huu,” alisema Batakanwa.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment