Tuzo hiyo iitwayo “The African Youth Peace Award”, hutolewa na umoja huo kwa wakuu wa nchi na viongozi wa Afrika, ambao wamethibitika kuchangia kwa kiasi kikubwa ustawi wa Waafrika.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, ilisema jana kuwa , Rais Kikwete alikabidhiwa tuzo hiyo na Rais wa Umoja huo, Francine Muyumba, wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).
Alikabidhiwa tuzo hiyo aliposimama kwa dakika chache kuwasalimia vijana wanaohudhuria mkutano wa tatu wa viongozi vijana wa Afrika na China, mkoani Arusha.Muyumba alimweleza Rais Kikwete kama kiongozi mfano wa kuigwa kwa mchango wake katika kuwatambua na kuwaendeleza vijana katika nafasi za uongozi.
Rais Kikwete alikutana kwa mazungumzo na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), ambaye pia ni Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, aliyekuwa jijini Arusha kufungua mkutano huo.
Alimshukuru Rais Mugabe kwa kukubali mwaliko wake wa kutembelea Tanzania ili kufungua mkutano huo.
Rais Kikwete pia alikutana kwa mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Wang Jiariu, ambaye ndiye kiongozi wa msafara wa vijana kutoka China kwa ajili ya mkutano huo.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment