Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, vijana hao walisema Dk. Kahangwa ni miongoni mwa watu ambao walibainika kuwa na sifa kati ya watu waliofikiliwa na kitengo cha vijana cha Chama hicho.
Mwingine ambaye waliesema waliona anafaa ni Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia (pichani), ambaye baada ya kumuomba kuwania nafasi hiyo hakuwa tayari na kueleza kuwa kwa sasa Jimbo la Vunjo, mkoani Kilimanjaro linahitaji msaada wake.
Mwenyekiti wa Kitengo cha Vijana Taifa, Deo Meck, alisema wanaamini Dk. Kahangwa atakuwa ni miongoni wa wagombea wazuri wa nafasi hiyo, watakao pambanishwa katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).Meck alisema Dk. Kahangwa amekuwa mwanachama na mwanamageuzi wa siku nyingi, ni msomi wa kiwango cha juu na mwenye vipaji vingi visivyofungwa na mipaka ya taaluma na ana sifa za uongozi.
“Tumeamua kuwa licha ya kumwomba akubaliane na pendekezo letu, tumefanya kama surprise (kushtukiza) ya kumuomba agombee nafasi hii pasipo kumshirikisha kwanza kwa sababu tunaamini kwamba ni mzalendo hawezi kukataa, tukitoka tutaenda moja kwa moja nyumbani kwake kumpelekea taarifa hizi,” alisema Meck.
Aliongeza: “Tutafanya jitihada za kuhakikisha jina lake linafika katika kikao cha Halmashauri ya chama, kupewa baraka za mkutano mkuu wa chama, sisi vijana tutamchukulia fomu ya chama ya kuwania nafasi hiyo muda utakapofika na tutalipa wenyewe na hatimaye aende kushindanishwa na wagombea na wengine wa Ukawa.”
Meck alisema uamuzi wa vijana hao wa kupendekeza mgombea wanayemtaka ni wa kwao binafsi na si wa chama, na haimaanishi kuwa wengine wasijitokeze kuwania nafasi hiyo.
“Ieleweke kwamba sisi kama vijana tumeamua kupendekeza mtu tunayeona anatufaa kulingana na sifa alizonazo, haimanishi kwamba tunawafungia watu wengine milango wanaohitaji kuwania,” alisema.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment