Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, March 5, 2015

Zitto Kabwe ashangaa uzushi wa Ngeleja

Mwenyekiti Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serilali (PAC) na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.
Mwenyekiti  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serilali (PAC) na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, amejibu tuhuma zilizoelekezwa kwake na Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja, kwamba naye amekuwa akipokea misaada mbalimbali kwa matumizi binafsi kuwa ni upuuzi.
 
Zitto alijibu tuhuma hizo jana kupitia ukurasa wake wa Facebook, ikiwa ni siku moja baada ya Ngeleja kumtuhumu na kueleza kuwa tuhuma hizo ni za kipuuzi na kwamba ameshawahi kuzijibu huko nyuma na kuziita ni siasa za majitaka.
 
“Tuhuma zote hizo zimeshawahi kutolewa huko nyuma, hazina msingi wowote na zilikuwa siasa za majitaka, hata hivyo zimekuwa zikijirudia rudia kwa malengo maalumu wanayoyajua wanaotoa tuhuma hizo” alisema Zotto na kuongeza: “Watuhumiwa wa ufisadi wa Escrow hawajazoea kuona taasisi za maadili zikifanya kazi kwa namna ilivyo sasa, hivyo wanajaribu na wataendelea kubwabwaja na kuhangaika ikiwamo kutaka kila mtu aonekane ni mtuhumiwa kama wao.”
 
“Ndiyo maana Ngeleja ametaja msururu wa watu akiwamo mfanyabiashara kwamba huwapa fedha wabunge bila kuwapo chembe ya ushahidi, hivyo narudia kutamka kwamba ninataka uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo ufanyike mara moja, wenye ushahidi wapeleke katika vyombo vya uchunguzi na niitwe mbele ya Baraza la Maadili kujieleza,” alisema Zitto.
 
Aidha, Zitto aliunga mkono kazi iliyofanywa na Baraza la Maadili, alieleza kazi hiyo ilipaswa kuwa imefanywa kwa muda mrefu sasa kwa kashfa mbalimbali zilizowahi kuwapata viongozi, kama vile rada, rushwa katika manunuzi ya mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya umeme, kujipatia mikopo katika taasisi za umma bila kulipa na kujilimbilikizia mali tofauti na kipato.
 
Zitto aliiomba Sekretarieti ya Maadili izichukulie kwa uzito tuhuma za Ngeleje dhidi yake, kwani kwa mujibu wa sheria na kanuni za utumishi wa umma yanapaswa yafanyiwe uchunguzi. 
 
Akijitetea juzi kwenye Baraza la Maadili, Ngeleja alikiri kupata mgawo wa Sh. bilioni 40.2 kutoka kwa mfanyabiashara James Rugemalila wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd na kudai kuwa wabunge wamekuwa wakifadhiliwa na wafanyabiashara na  mmoja wa wabunge walionufaika na misaada ya fedha za wafadhili, ni Zitto, ambaye kisheria ni mtumishi wa umma.
 
Alidai Zitto alinufaika na msaada wa zaidi ya Sh. milioni 30 na dola za Marekani 5,000 kutoka kwa Kampuni ya Pan Africa Power (PAP) na Independent Power Tanzania Limited (IPTL) alizopata kwa matumizi yake binafsi.
 
Ngeleja alidai misaada mingine, ambayo Zitto amewahi kuipata ni pamoja na unaohusu Sh. milioni 119.9 na Sh. milioni 79, ambayo alidai kuwa aliipata kutoka Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). 
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment