Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kintintu mara baada ya kuzindua tawi la chama hicho.
Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe na Mwenyekiti wa Chama hicho Anna Mghwira wakizindua tawi la chama hicho kwenye Kijiji cha Kintintu wilayani Manyoni mkoani Singida.
Wakazi wa Mji wa Singida wakishangilia viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo wakati waa mkutano huo jijini humo leo.
Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Anna Mghwira, akiwahutubia wakazi wa Manyoni Mjini.
Wakazi wa Manyoni wakipiga picha na simu zao.
Zitto Kabwe akisalimiana na wak
Katika mazungumzo yake Zitto amesema ACT kinaweza kuunganisha nguvu na vyama vingine vya upinzani ili kukiondoa chama cha mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu ujao ambapo alisema shauku kubwa ya wananchi ni kutaka kujua msimamo wa ACT Wazalendo katika kushirikiana na vyama vingine vya siasa ili kufanikisha malengo ya kuiondoa CCM katika madaraka.
Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Singida na Kiongozi wa ACT wazalendo Zitto Kabwe wakati akihutubia mamia ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi ukombozi."Tumedhamiria kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa kuubomoa mfumo unaonyonya wananchi. Msimamo wetu upo wazi na tumeueleza mara kadhaa"alisema na kuongeza
“ACT- Wazalendo tunaunga mkono juhudi zozote za kushirikiana kwa vyama na hili linathibitishwa na jina letu Alliance na msimamo wetu kuhusu mabadiliko ya Katiba. Kubwa tunataka ushirikiano utakaonufaisha wananchi na sio ushirikiano wa kugawana nafasi za uongozi,” alisema Zitto.
Kiongozi huyo wa ACT alisema chama hicho hakina tatizo na kipo tayari kushirikiana na chama chochote kilichokuwa tayari kushirikiana nao ikiwemo Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

No comments :
Post a Comment