Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, April 11, 2015

Hofu ya ugaidi kupitia mitandao yatawala Arusha.

  Polisi yataka wananchi wapuuze ujumbe huo.

Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Liberatus Sabas.
Hofu ya ugaidi imetawala mkoani hapa, kufuatia kusambaa kwa ujumbe mfupi kwenye mitandao ya kijamii na simu za kiganjani kuwa kuna magaidi wanne wamekamatwa na silaha aina ya SMG katika chuo cha Uhasibu Njiro (IAA). 
 
Akizungumzia taarifa hizo, Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Liberatus Sabasi, alisema wananchi wanapaswa kuendelea na shughuli zao kama kawaida na kupuuza ujumbe huo.
 
“Ujumbe huo ulikuwa na lengo la kuwatia hofu wananchi, sio kweli na sisi watu wa ulinzi na usalama tumeimarisha ulinzi, watu wafanye kazi zao kama kawaida,”alisema.
 
Alisema taarifa hizo zitakuwa zimesambazwa na wahuni wachache kwa lengo wanalojua wenyewe.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Ntibenda, alipopigiwa simu ya kiganjani, alisema taarifa hizo zilizosambazwa ni za uongo na kutaka watu wazipuuze.“Mimi nipo katika kikao sasa hivi cha kamati ya ulinzi na usalama, hizo taarifa za uongo na uzushi mkubwa watu wazipuuze,” alisema.
 
 Afisa habari wa Chuo cha Uhasibu Njiro, (IAA), Sarah Goroi, akizungumza kwa njia ya simu ya kiganjani, alikanusha uvumi huo na kudai wanafunzi wanaendelea na masomo kama kawaida.
 
“Taarifa hizo hazina ukweli wowote, tunaomba wafunzi waendelee na masomo yao kwani huo ni uzushi,”alisisitiza.
 
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) , Gasto Leseiyo, alisema  chuo chao katika kukabiliana na magaidi wamefunga kamera maalum za kutambua wahalifu na sasa wameanza kuzifunga maeneo ya nje ya chuo baada ya kukamilisha kazi hiyo ndani ya chuo.
 
Mmoja wa wakazi wa Jiji la Arusha, Samwel Mollel,  alisema kuwa taarifa hizo zisipuuzwe zifanyiwe kazi, kwani hali ya usalama sasa ni tete na wananchi lazima wawe na mashaka kutokana na kilichotokea Garissa nchini Kenya.
 
Mapema asubuhi jana, kulisambazwa ujumbe wa maneno kwenye simu za mkononi, ukidai kuwa maafisa usalama Arusha, usiku wa kuamkia jana, wamekamata watu wanne wakiwa na gari aina ya Premio nyeusi ikiwa na bunduki SMG nne na risasi 160. 
 
Watu hao walikuwa wakijaribu kuingia chuo cha Uhasibu Njiro kwa madai ya kutaka kusalimia mwanafunzi mmoja wa kike ambaye ni ndugu yao, kisha kutiliwa mashaka na kutiwa mbaroni.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment