Na Rashid Abdallah
Ijumaa iliyopita hakimu Alvin Hellerstein, ameitaka serekali ya Marekani kuzitoa picha zaidi ya 2,000, zinazoonesha mateso yaliyofanywa na Majeshi ya Marekani huko Iraq na Afghanistan wakati wa utawala wa Bush.
Hayo yamekuja baada ya serekali ya Marekani kushindwa kuthibitisha kuwa kuziachia picha hizo kunaweza kuhatarisha usalama wa Marekani. Pia imetakiwa kuziweka hadharani picha hizo ikiwa ni jawabu ya kuheshimu sheria ya uhuru wa habari.
Naibu Mkurugenzi wa sheria katika, shirika lisilo la serkali la The American Civil Liberties Union (ACLU), linalotetea uhuru,haki na usawa wa mtu mmoja mmoja kwa kufuata katiba na sheria za Marekani, anasema: “Picha hizo ni muhimu kwa umma, ni ushahidi bora wa kile kilichofanyika katika vituo vya kijeshi. Kuoneshwa kwa picha hizo ingesaidia umma kuelewa vizuri maana halisi ya baadhi ya sera za utawala wa Bush”.Shirika hili linataka walimwengu waone hasa kile kilichofanyika kule Iraq, kuanzia mwaka 2003, hasa katika gereza la Abu Graib . Ukweli wa mambo ni kuwa Bush rais mstaafu wa Marekani alistahili na bado anastahili kupelekwa katika mahakama ya ICC, kwenda kujibu yale aliyoyafanya Iraq,Afghanistan na maeneo mengine.
Muda ukifika nitakupa baadhi ya matukio na kukuhadithia baadhi ya picha chache ambazo zimevuja kutoka katika gereza hilo, na mazungumzo ya mmoja wa wafungwa walioshikiliwa katika gereza hilo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa makala ya televisheni.
Unyama mkubwa na wa kutisha umefanyika na serekali ya Marekani tangu ilipoamu kuivamia Afghanistan, na uvamizi wa Iraq mwaka 2003 yamefanyika mengi ya unyama. Kama vile yaliyofanyika Vietnam miaka hiyo na Majeshi hayo hayo ya Marekani.
Mtandao wa Occupy Democrats, wa shirika linalopambana na matabaka na ukosefu wa usawa huko Marekani, April 8, mwaka huu,linasema; “Mwaka 2009 serekali ya Marekali ilijaribu kuibadilisha kwa siri kwa kushirikiana na bunge la Marekani-Congress sheria ya uhuru wa habari (Freedom of Information Act), ili iyendelee kuzificha picha hizo”.
Rais Barack Obama aliwahi kukubali kuziachia picha hizo lakini kisha akabadilisha uwamuzi wake, na kusema zisitolewe. Bado tu anaendelea kumfichia mtangulizi wake, unyama alioufanya Iraq na Afghan.
Ukweli hadi sasa bado wanaendelea kuzificha. Wanaficha unyama waliowafanyia binaadamu. Katika gereza la Abu Graib binaadamu waliteswa sana na kudhalilishwa kingono na aina nyengine za mateso ya kutisha yasiyostahili binaadamu.
Kwa sasa hali mbaya zaidi inaonekana kuendelea kule Guantanamo Bay, muongo mmoja wa uvamizi wa Marekani Afghanistan, umepelekea mamia ya vijana kushikiliwa katika gereza hilo la jahannam. Gereza la wababe wa kutesa.
Moja ya video ambayo watetezi wa haki za binaadamu wanataka itolewe ni ile inayowaonesha watoto wa kiume wakiingiliwa kinyume na maumbile, mbele ya Mama zao katika gereza la Abu Ghraib huko Iraq.
Watoto hao waliingiliwa huku askari wa Kimarekani akichukua kwa mkanda wa video tukio hilo la kinyama. Kulikuwa na baadhi ya barua ambazo zilipenya kutoka kwa wanawake katik gereza hilo kwenda kwa jamaa zao nje, barua zilikuwa zikiwataka jamaa wa wanawake hao waende wakawaue, kutokana na waliyofanyiwa ama kuyaona huko gerezani.
Mwandishi mchunguzi Seymour Hersh, aliyefichua mauaji ya raia katika vita vya Vietnam yaliyotekelezwa na wanajeshi wa Marekani, vita ambavyo wanawake walikuwa wanabakwa kwa mtungo na wanajeshi wa Marekani, kisha miili yao inakatwa katwa. Mwandishi huyo aliyefichua unyama huo, pia aliripoti kuwa; The USA military was sodomizing children in Iraq on video back 2004.
Nyingi ya picha hizo zilikuwa zinapigwa na wanajeshi wenyiwao wakati wakitesa na kufanya mauji kwa wafungwa, kuwabaka, kuwaigilia kinyume na maumbile, kuwatesa kupitilza . Ripoti za maandishi zilizotolewa na Amnesty International na Associated Press mwishoni mwa mwaka 2003, ndizo ripoti za mwanzo zilizofichua unyama huo.
Picha ya Ali Shallal al-Qaisi, wakati akiteswa ndio picha maarufu kwa jamiii ya kimataifa, ambayo ndiyo ya mwanzo kufichua kashfa ya wanajeshi wa Marekani huko Abu Graib, picha hii ilipatikana April 2004. Ali Shallah ni Muiraq aliyekuwa mfungwa katika gereza la Abu Graib.
Picha hiyo inamuonesha mtu aliyesimama juu ya sanduku, mikono yake ameinyoosha kulia na kushoto, akiwa katika vazi jeusi na kichwa chake na uso vikiwa vimefunikwa kofia nyeusi, huku waya za umeme zikiwa zimewekwa katika vidole vyake.
Ali Shallah alipokuwa anahojiwa katika makala ya “Abu Graib Prison-Iraq: Barbaric Touture & Abuse of Iraq Prison by The American’s” iliyotolewa na Javed Khan Dawlataza, anasema wakati ule alikuwa anahisi kama macho yake yanatoka nje, anajiuliza kuwa alikuwa binaadamu ama taa ya umeme (bulb).
Baadhi ya picha ambazo zimevuja, pia ipo ile inayowaonesha wanaume walio utupu wa mnyama wakilazimishwa kujitoa manii mbele ya wanajeshi wa kike huku tukio hilo likichukuliwa kwa kamera.
Ipo pia picha ya mtu aliyepewa jina la “shit boy” na wanajeshi wa Marekani, hii ni picha ya mtu aliyelazimishwa kujisaidia haja kubwa kisha akatakiwa ajipake mwilini mwake na uso pia. Huku akiwa utupu wa mnyama.
Wapo waliokojolewa na kulazimishwa kunywa mikojo ya wanajeshi. Ali Shallah anasema wapo wanaume waliobakwa mbele ya wake zao, pia wapo wake waliobakwa mbele ya waume zao, pia wapo wanawake waliongiliwa mbele ya familia zao.Taarifia pia zinasema wapo wanawake walibakwa na kushika mimba.
Hizo ni baadhi ya picha na matukio machache ambayo yamevuja, lakini bado kuna mamia ya picha ambazo serekali ya Marekani wamezishikilia na hawataki kuzitoa, hawataki watu waone unyama walioufanya, hawataki watu wasikie walichokifanya, hawataki tuone unyama wao.
Taarifa zinasema kuwa serekali ya Marekani inayo miezi miwili ya kuamua kukata rufaa na kuendelea kuuficha ukweli uliokwenda kinyume na haki za binaadamu katika utawala wa Bush.
Upo ugumu wa kufikiria kuwa huenda Marekani wakaamua kuzitoa picha hizo, ukweli ni jamboa gumu kwa serekali ya kibabe kama Marekani kufichua unyama wao. Naamini wasipozitoa leo basi kesho zitafichuka, wapo watakao tokea na kufichua kama vile alivyofanya Edward Snowden.
Muandishi mmoja aliwahi kuuliza hivi; Wako wapi watesa na wateswaji? Kisha akatolea mifano ya tawala za kibabe ambazo zimekufa na wababe pia hawapo tena, pia aliwataja baadhi ya wateswaji nao pia hawapo tena.
No comments :
Post a Comment