TAARIFA za kundi la kigaidi la Al-Shabaab kutekeleza shambulio katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha jana zilizua taharuki kubwa katika baadhi ya taasisi, vyuo na maeneo mengine, huku baadhi wakibaki wasijue la kufanya.
Hofu kubwa ilitanda jana katika maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo, kutokana na ujumbe ambao umekuwa ukisambazwa muda mrefu kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii na simu za mkononi, ukidaiwa kutolewa na Umoja wa Mataifa (UN), ukiwatahadharisha watu kukaa mbali na mikusanyiko ya watu siku ya Ijumaa (jana) na leo Jumamosi ili kuepuka shambulizi la kigaidi.
Taarifa zilizokusanywa na gazeti hili katika maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo, hususani mahotelini, vyuoni na kwenye mikusanyiko ya watu iliyotajwa kulengwa kama ilivyoelezwa katika taarifa hiyo ambayo hata hivyo imekanushwa vikali na UN na Jeshi la Polisi, zimeonyesha kulikuwa na hali ya wasiwasi ambayo ilitanda kila kona.

DAR ES SALAAM
Katika jiji la Dar es Salaam, Jeshi la Polisi lilitoa angalizo likimtaka kila mmoja kuchukua tahadhari.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleimani Kova, alisema hawawezi kudharau taarifa zozote ziwe za ugaidi au za kawaida, hivyo walikuwa wameimarisha ulinzi katika maeneo yote yenye mikusanyiko ya watu, ikiwa ni pamoja na nyumba za ibada.
“Ninatoa agizo kwa wafanyabiashara wote wakubwa kama vile Supermarket, mabenki, maduka makubwa na mahoteli makubwa kufunga CCTV Camera na kuwa na vifaa vya kisasa vya ukaguzi katika biashara zao pamoja na kufunga mashine kwa ajili ya kuwakagua watu wanaofika katika maeneo hayo,” alisema Kova.Katika jiji la Dar es Salaam, Jeshi la Polisi lilitoa angalizo likimtaka kila mmoja kuchukua tahadhari.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleimani Kova, alisema hawawezi kudharau taarifa zozote ziwe za ugaidi au za kawaida, hivyo walikuwa wameimarisha ulinzi katika maeneo yote yenye mikusanyiko ya watu, ikiwa ni pamoja na nyumba za ibada.
Wakati Kova akisema hayo, hali hiyo ya wasiwasi ilisababisha baadhi ya wanafunzi, hususani wa vyuo kutofika kabisa madarasani na wengine wakiondoka na kurudi majumbani kwao.
Hali hiyo inatajwa kuvikumba vyuo karibu vyote vya jiji hilo, vikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo Kikuu cha Tumaini tawi la Dar es Salaam na vingine.
Si hivyo tu, hata katika baadhi ya maofisi, kulikuwa na hali ya kuchukua tahadhari kiasi cha kulazimu kuanzisha utaratibu mpya wa kukaguliwa wafanyakazi pamoja na wageni.
Shirika la Umeme (Tanesco) lilitoa tangazo likiwataka maofisa wao wa usalama wa kila mkoa, hasa iliyotajwa kuchukua tahadhari za kiusalama kuhakikisha kila mtu anayeingia kwenye majengo au ofisi zao kukaguliwa na kuandikishwa kwenye kitabu cha wageni pamoja na kuhakiki mgeni anakokwenda.
Ofisa Uhusiano wa Tanesco, Adrian Mvungi, alipotafutwa alisema tahadhari hiyo wameichukua, kwani hata Jeshi la Polisi tayari limetoa angalizo hilo.
Taarifa zinazofanana na hizo ambazo gazeti hili limezipata zinaeleza kuwa, baadhi ya vyombo vya usalama vilikwisha
kuwatangazia wafanyakazi wake kuchukua tahadhari kokote watakapokuwa.
Mtoa taarifa huyo alisema kuwa hali hiyo ilitokana na hofu ya matukio ya kigaidi yaliyoikumba nchi jirani ya Kenya hivi karibuni.
Hata hivyo, tofauti na kauli kama hizo, uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika maeneo mbalimbali ya jiji ulibaini kuwa
katika baadhi ya maeneo, husuani baadhi ya hoteli na vyuo vikuu hakukuwa na ulinzi imara.
ARUSHA
Jijini Arusha hali ya taharuki iliwakumba baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu kiasi cha kulilazimisha Jeshi la Polisi kukesha likiwalinda wanafunzi hao juzi usiku, huku wengine wenye ndugu na jamaa zao wakiondoka na kulala nje ya chuo hicho.
Hali hiyo ilikuja baada ya uvumi kusambaa katika mitandao ya kijamii kuwa maofisa wa usalama wakishirikiana na polisi walikuwa wamekamata gari dogo jeusi aina ya Toyota Premio likiwa na watu wanne waliokuwa na bunduki nne aina ya SMG na risasi 160, wakitaka kuingia katika geti la chuo kabla ya kutiliwa shaka na walinzi ambao walitoa taarifa kwa vyombo vya usalama.
Ujumbe huo ambao hata hivyo ulikanushwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha, ulidai kuwa; “Watu hao walijifanya ndugu wa mmoja wa wanafunzi wa kike anayeishi kwenye hosteli zilizopo ndani ya campus. Walinzi wa getini waliwatilia shaka ndipo walipotoa taarifa kwa siri Polisi na haraka walitiwa nguvuni hapo hapo. Chukueni tahadhari”.
Taarifa hizo ambazo zilisambaa kwa kasi chuoni hapo zilisababisha wanafunzi wa chuo hicho kuanza kukimbia na kupiga kelele ovyo.
Licha ya Jeshi la Polisi kufika kwa ajili ya kuwahakikishia usalama wao, baadhi ya wanafunzi waliondoka pasipo kujali maandalizi ya mitihani yao.

“Hali ilizidi kuwa mbaya kuanzia saa moja na nusu usiku, wengi wetu kutokana na woga na jinsi tulivyoona wenzetu wa Garisa (Chuo Kikuuu cha Garisa kilichoshambuliwa na wanafunzi 148 kuuawa huko Kenya) ilibidi tukimbie kujiokoa, ni tukio la kutisha huwezi kusubiri kifo kikukute,” alisema mmoja wa wanafunzi anayesoma chuoni hapo, ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
Tangu uvumi huo usambae, Jeshi la Polisi pamoja na vyombo vingine vya usalama vimeendelea kushika doria katika viunga vya Jiji la Arusha kuhakikisha wananchi wanaishi na kufanya shughuli zao bila hofu.
Ofisa Habari wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), Gaston Leseiyo, alisema
katika kulinda hali ya usalama chuoni hapo, wanazo kamera za ulinzi na wanatarajia kufunga kamera nyingine kuzunguka chuo kizima.
Wakati baadhi ya wakazi wa Arusha wakikumbwa na hali hiyo ya wasiwasi, kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa iliitishwa ili kujadili tishio hilo la ugaidi.
Akizungumza kwa kuhamaki huku akionekana kujawa na fadhaa kutokana na uvumi huo uliovikosesha usingizi vyombo vya ulinzi na usalama na kusababisha sintofahamu kwa wakazi wa Arusha, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda (Kijiko), alisema hizo taarifa ni za uzushi na uongo.
Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema
huo ni uzushi ambao umetengenezwa na wahuni wachache, ingawa alisema wameimarisha ulinzi kila kona ya jiji hilo kufuatia madai hayo.
Baadaye jana mchana, Mkuu huyo wa Mkoa, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, aliwataka wamiliki wa hoteli kuhakikisha kuwa wanasajili wageni wanaofika kwenye hoteli zao kwa kuzingatia utaratibu, ikibidi waonyeshe na vitambulisho vyao.
Pia aliwataka watendaji wa Serikali za Mitaa na vijiji kuhakikisha wanatambua wageni wanaoingia kwenye maeneo yao.
“Nyumba za ibada, yaani makanisa na misikiti, kwenye mikusanyiko ya watu, vyombo vya dola vimeimarisha ulinzi, suala hili la ulinzi tumejipanga kukabiliana na uvunjifu wowote wa amani unaoweza kujitokeza, Arusha tuko salama na tunakaribisha wageni kwetu.”
Alipoulizwa kuhusiana na chanzo cha ujumbe huo ambao unasambaa kwenye mitandao, alisema kuwa suala hilo linafuatiliwa kwa ngazi ya Taifa na Mkoa pia kwa lengo la kubaini aliyeanza kusambaza ujumbe huo.

Akizungumzia hali ya mipaka, Mkuu huyo alisema kuwa wameimarisha ulinzi kwenye mipaka kwa kutumia Intelijensia.
Katika muktadha huo huo, Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Dar es Salaam lilitoa taarifa likionya tabia iliyoibuka kwa baadhi ya watu wachache wasiofahamika kutunga na kusambaza ujumbe kupitia simu za mikononi na mitandao mbalimbali ya kijamii wenye lengo la kuwatia hofu wananchi, jambo lililodai kuwa ni kinyume cha sheria.
“Jeshi la Polisi nchini linawataka wote wenye tabia hiyo kuacha mara moja na badala yake, endapo mtu yeyote anayo taarifa ya uhalifu wa aina yoyote ama kikundi chochote cha uhalifu atoe taarifa hiyo katika kituo chochote cha Polisi au kupitia simu za makamanda wa polisi wa mikoa ama vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili taarifa hizo ziweze kufanyiwa kazi haraka,” ilieleza taarifa hiyo, iliyosainiwa na Msemaji wa Jeshi hilo, Advera Bulimba.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi lilisema halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kusambaza ujumbe wenye lengo la upotoshaji, uchochezi ama kuwatia hofu wananchi.
Zaidi Jeshi hilo lilisema linaendelea na uchunguzi wa taarifa zote zinazopokelewa ili kuhakikisha kwamba usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika.

No comments :
Post a Comment