Hatua hiyo ina lengo la kudhibiti ugomvi wa mara kwa mara kati ya wafuasi wa CCM na CUF.
Akizungumza na waandishi wa habari visiwani hapa, mkuu wa upelelezi na makosa ya jinai Zanzibar, Salum Msangi, alisema agizo hilo limefuatia tukio la hivi karibuni ambapo wafuasi wa CUF walishambuliwa na watu wasiojulikana.
Akitoa ufafanuzi huo alisema tayari jeshi hilo limeshakaa pamoja na viongozi wa vyama vya siasa na kukubaliana na kuweka maadhimio ambayo atakaekiuka atachukuliwa hatua za kisheria.
Alitaja maadhimio hayo ni pamoja na kufuata sheria za usalama wa barabarani, kuepuka kupakia watu katika magari kupita kiasi, kuepuka kufanya maandamano kabla na baada ya mkutano na kuepuka kuandika mabango yenye ujumbe wa matusi na yanayoashiria uvunjifu wa amani.
“Tukiwa tunaelekea katika uchaguzi mkuu tumekuwa tukishuhudia viashiria vya uvunjifu wa amani katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuchomwa moto majengo ya vyama vya siasa, wafuasi kujeruhiwa na mabango yenye ujumbe tofauti ambao unaashiria uvunjifu wa amani,” alisema Msangi.

Alisema kama vurugu zitaendelea wataishauri serikali kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa mpaka tume ya uchaguzi itakapotangaza kufanya mikutano kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mkuu.
Alisema maadhimio hayo endapo yatatekelezwa wataepusha ajali za barabarani, kuendelea na hali ya amani na utulivu na kuzuia fujo katika maeneo ambayo misafara hiyo hupita kutokana na mihemko, jazba za kiasia.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment