Msipa wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Pandu Ameir Kificho akiwasili katika jengo la Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar kwa ajili ya kuendesha Mkutano wa Baraza la Wawakilishi kusomwa hutuba ya Bajeti ya mwaka 2015-2016.
Spika wa Baraza la Wawakilishi akisalimiana na Wafanyakazi wa Baraza baada ya kuwasili katika viwanja vya Baraza.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akiwasili katika Jengo la Baraza la Wawakilishi kuhudhuria Mkutano wa Baraza kuwasilishwa Bajeti ya Serikali na Mhe Omar Yussuf,
Mwakilishi wa Jimbo la Kwani Zanzibar Mhe Ali Salim akiingika katika Ukumbi wa Mkutano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe. Said Ali Mbarouk na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Abubakar Khamis Bakar wakiingia katika ukumbi wa mkutano.
Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe. Omar Yussuf Mzee akisoma Hutuba ya Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakati wa Kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuwakalisha Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2015-2016.
Waheshimiwa wakifuatilia Bajeti wakati ikisomwa na Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee.
Waheshimiwa wakiwa makini kufuatilia Hutuba ya Bajeti wakati ikisomwa katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi.
Mabalozi Wadogo wanaowakilisha Nchi Zao Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Bajeti katika vitabu vyao wakati ikisomwa na Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee.
Watendaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Bajeti
Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Bajeti wakati ikiwakilishwa na Waziri husika wa Wizara ya Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee. I
Waziri wa Fedha wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Saada Mkuya akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar Ndg Khamis Mussa, wakiwa katika ukumbi wa Mkutano wa Baraza.
Wadau wa Maendeleo wakifuatilia hutuba ya Bajeti kwa mwaka 2015-2016.
Chanzo: ZanziNews
No comments :
Post a Comment