Mkutano huo ambao Naibu Katibu Mkuu Bara wa chama hicho, Magdalena Sakaya alitarajiwa kuwahutubia mamia ya wakazi wa manispaa hiyo wakiwemo makada wa chama chake.
Songea. Polisi mjini Songea, imezuia mkutano wa Chama cha Wananchi (CUF) uliokuwa ufanyike kwenye Viwanja vya mikutano vilivyopo eneo la Majengo Manispaa ya Songea.
Mkutano huo ambao Naibu Katibu Mkuu Bara wa chama hicho, Magdalena Sakaya alitarajiwa kuwahutubia mamia ya wakazi wa manispaa hiyo wakiwemo makada wa chama chake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alipopigiwa simu na mwandishi wa gazeti hili kwa lengo la kutaka ufafanuzi alisema kuwa hana taarifa zozote na alipomuuliza mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Songea(OCD) naye alikataa kuwa hana barua ya aina yoyote ya CUF ya kuomba kufanya mkutano na amewataka wafuate taratibu zinazotakiwa na wakitaka kuanzia kesho wafanye mkuatano hata kwa siku kumi.
Baadhi ya Waandishi wa habari ambao walifika kwenye eneo la tukio akiwemo mwandishi wa gazeti hili kwenye viwanja hivyo vya mikutano na kukuta hali ya sintofahamu baada ya baadhi ya makundi ya watu yakiendelea kulalamika kuzuiliwa kufanyika kwa mkutano huo ambao baadhi ya viongozi wa chama hicho waliwaeleza waandishi wa habari kuwa mkutano huo ulikuwa na lengo la kusaidia kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi katika kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la kupiga kura na si vinginevyo.
Katibu wa chama hicho wa Wilaya ya Songea Khamis Khais alipohojiwa na waandishi wa habari alisema kuwa tangu Aprili 29 mwaka huu chama chake kiliandika barua ya kuomba kibali cha kufanya mkutano wa nje kwenye viwanja vya majengo kwa jeshi la polisi kituo kikuu cha Songea ambapo barua hiyo ilipokelewa na kusainiwa kwenye kitabu chao cha CUF (dispachi ) na kujibiwa kwa mdomo kuwa wakaendelee kufanya mkutano huo jambo ambalo CUF imetekeleza kwa kuwahamasihsa wananchi wahudhurie kwa wingi kwenye mkutano ambao umezuiliwa hata kabla ya kuanza licha ya wananchi wameshafika kwenye viwanja hivyo.
No comments :
Post a Comment