zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, July 19, 2015

MAONI KUHUSU NEC NA ZEC KUTOKA MZALENDO.NET!

Image result for zanzibar electoral commission
Image result for zanzibar electoral commission

(TUNAYATOA MAONI HAYA YA MZALENDO KWASABABU NI KWELI HALI HAITAMBULIKI MPAKA SASA - ZNK)
Leo ni skukuu ya pili, mambo yanaanza kuchemka. Tulikuwa na mzee wetu Abdi Salim kipindi sasa hatujamsikia. Pengine ni uzee umemzidi au kafa kihoro. Alaaa kulli hali, mamlaka kamili ya Zanzibar yanahitji kupiganiwa.

Nirudi kwenye lengo la leo ni mchanganyiko wa ukatwaji wa majimbo. Wananchi wengi hawafahamu jee Zanzibar kuna majimbo mangapi ya uchaguzi? Au Zanzibar itatowa wabunge wangapi uchaguzi wa 2015?

Hili limetokana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC kuongeza majimbo 4 kwa upande wa Unguja na kufikisha idadi ya majimbo 54 kwa Zanzibar nzima. Haina mushkeli kwa vile ZEC ndio chombo chenye mamlaka ya kuongeza amma kupunguza majimbo ndani ya Zanzibar.

Kwa upande wa pili wa sakata nikusikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi nayo ikiongeza majimbo 26 kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2015 bila ya kuyajumuisha na haya 4 yaliyoengezwa Zanzibar.

Huku kukiwa na fununu kwamba NEC haitambui ongezeko hili la majimbo ya Zanzibar.Hapo ndio mchanganyiko wenyewe ulivyo. Bahati mbaya suala hili halijazungunzwa kwa kina na wananchi wakafahmishwa hali ya kuwa linawaathiri hasa watia nia ya kugombea nafasi ya ubunge kwa majimbo yaliyoongezwa. Hapo itakuja suala kwani ni jimbo lipi limeongezwa? Jawabu halijulikanwi. Kwani mengi yamebadiliahwa majina na mipaka.

Tukisema jimbo la Malindi ni jipya ndio limeongezwa, hivyo Mbunge wake hatambulikanwi na NEC itakuwaje?

Kwa utata huu ndio ninapoona ZEC inakuwa kikarogosi kinachotumikia bwana wake mkoloni ambaye ni NEC. Muda mrefu ZEC ilikuwa na mchakato wa uhakiki wa majimbo, ikiwakusanya wadau na kuwashirikisha wanachi watoe maoni yao. NEC ILIKUWEPO WAPI? Hata ije sasa na ikatae ongezeko hili.

Wakati umefika wa kadhia kuzungumzwa kwa kina na tupewe jawabu sasa kabla ya hatujaingia kwenye kampeni.



No comments :

Post a Comment