Mwakilishi wa Benki ya Dunia Nchini Tanzania Bibi Bella Bird akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwa Balozi Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Ujumbe wa Benki ya Dunia { WB } uliofika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kubadilishana nao mawazo. Kulia ya Balozi Seif ni Kiongozi wa Ujumbe huo Mwakilishi wa Benki ya Dunia Nchini Tanzania Bibi Bella Bird.(Picha na –OMPR – ZNZ).
Na Othman Khamis Ame, OMPRMakamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema ipo haja kwa wakulima Nchini kupatiwa taaluma ya kutosha na ya kisasa katika kukabiliana na Mabadiliko ya tabia Nchi yanayoonyesha muelekeo wa kuiathiri Sekta ya Kilimo Duniani.
Alisema Taaluma hiyo inayohitaji uwezeshwaji mkubwa kwa lengo la kufanikiwa vyema inapaswa kuungwa mkono ya Benki ya Dunia { WB } ili kuwapa faraja wakulima wanaofikia Idadi ya asilimia 80% ya watu wote Nchini Tanzania.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akizungumza na Ujumbe wa Maafisa wa Benki ya Dunia { WB } ukiongozwa na Mwakilishi wa Taasisi hiyo hapa Tanzania Bibi Bella Bird alipokutana nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo ndani na nje ya Nchi inajitahidi kuimarisha miundo mbinu katika sekta ya kilimo itakayowapa fursa pana wakulima kuongeza uzalishaji hasa katika kilimo cha umwagiliaji.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo ndani na nje ya Nchi inajitahidi kuimarisha miundo mbinu katika sekta ya kilimo itakayowapa fursa pana wakulima kuongeza uzalishaji hasa katika kilimo cha umwagiliaji.
Balozi Seif Ali Iddi alisema Taifa lazima liwe na chakula cha hakiba ya kutosha ili kujiweka tayari na upungufu wowote unaoweza kutokea kutokana na sababu za ukame, majanga na mabadiliko ya hali ya hewa.
Akizungumzia changamoto inayowakumba vijana wanaotumbukiza katika matumizi ya dawa za kulevya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuomba Uongozi huo wa Benki ya Dunia kuendelea kuisaidia Zanzibar na Tanzania kwa jumla taaluma pamoja na uwezeshaji wa kuambana na janga hilo.
Balozi Seif alisema kwamba nyumba za kurekebishia tabia kwa vijana walioathirika na dawa za kulevya zinahitaji gharama kubwa kisi kwamba Serikali pekee haiwezi kumudu kuzihudumia.
Mapema Mwakilishi wa Benki ya Dunia { WB } Nchini Tanzania Bibi Bella Bird alisema kwamba Taasisi yake imekuwa ikiangalia zaidi namna na mbinu za kuwasaidia Vijana katika nchi mbali mbali Duniani kumudu kuendesha maisha yao.
Bibi Bella Bird alisema hatua hiyo imelenga kuwakinga vijana wanaomaliza masomo yao wasitumbukie katika majanga mabaya na badaya yake wawe na maisha ya matumaini.
Alisema ipo baadhi ya Miradi inayosimamiwa na Benki ya Dunia Nchini Tanzania ambayo imeanzishwa kwa lengo la kuwawezesha vijana waingie ndani ya dunia ya mpya ya sayansi na teknolojia kwa kujiamini.
Alifahamisha kwamba Vyuo vya kuwajengea uwezo walimu wa masomo ya sayansi na lugha ni miongoni mwa mikakati ya Benki hiyo katika kuliandaa Taifa la Tanzania kuwa na wataalamu waliobobea katika fani ya sayansi hapo baadaye.
/ZanziNews.
No comments :
Post a Comment