Vijana wa Umoja wa Mapiki piki Wa CCM Wilaya ya Kaskazini “B” wakimsindikiza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akirehesha fomu za kuwania kugombea uwakilishi Jimbo la Mahonda.
Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi Fomu za kuwania kugombea Ujumbe wa Baraza la Wawakilushi Jimbo la Mahonda kwa Afisa wa Uchaguzi Wilaya ya Kaskazini “B” Nd. Makame Pandu Khamis ofisi ya Tume hiyo iliyopo Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wa Jimbo la Mahonda na vitongoji vyake wakiserebuka mbele ya Ofisi ya CCM Wilaya ya Kaksaini “B” wakati Balozi Seif akijiandaa kurejesha fomu alizochukuwa Tarehe 17 Agosti kutaka kuwania kugombea Uwkilishi Jimbo la Mahonda.
Balozi Seif akiwaunga mkono wanaCCM waliojitokeza kumuunga mkono wakati akirejesha fomu za kuomba kuwania kugombea Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Jimbo Jipya la Mahonda hapo Ofisi ya CCM Wilaya ya Kaskazini “B” Majonda.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na Othman Khamis OMPR.
Wakati harakati za uchukuwaji fomu za kuomba kugombea nafasi mbali mbali za Uongozi kwa wanachama wa vyama vya Siasa Nchini ukiendelea walipomaliza kuthibitishwa na vyama zao baadhi ya wanachama hao tayari wameanza hatua ya kurejesha fomu hizo kwa Ofisi za Tume za Uchaguzi za Wilaya baada kukamilisha kujaza fomu hizo.
Zoezi hilo lililoanza rasmi Mnamo Tarehe 17 Agosti mwaka 2015 na watarajiwa wanaohusika wakiingia katika Ofisi za Tume za Uchaguzi za Wilaya kwa makeke wakiambatana na wapambe wao linatarajiwa kuendelea hadi Tarehe 6 Septemba mwaka huu.Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amerejesha fomu za kuwania kugombea Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi katika Jimbo la Mahonda Wilaya ya Kaskazini “B” Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Akikabidhi fomu hizo Balozi Seif alimuhakikishia Afisa huyo wa Tume ya Uchaguzi kwamba kila alichojaza ndani ya fomu hizo ni sahihi wakiwemo wadhamini 48 licha ya utaratibu wa Tume hiyo kuhitaji wadhamini wasiopungua 25.
Akizipokea fomu hizo Afisa wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar { ZEC } Wilaya ya Kaskazini “B” Nd. Makame Pandu Khamis alisema kwamba jukumu ya Tume hiyo baada ya kupokea fomu zote ni kuhakiki fomu za wagombe wa ngazi zote kwa lengo la kukamilisha taratibu na kanuni zilizowekwa na tume hiyo.
Nd. Makame alisema watendaji wa Tume hiyo watabandika majina ya wagombea wote mbele ya ofisi hiyo baada ya kukamilisha uhakiki ili kuwapa fursa watakaohusika na mchakato huo kuangalia majina yao endapo kama kutakuwa na mapungufu yoyote.
Afisa huyo wa Tume ya Uchaguzi Wilaya ya Kaskazini “B” alieleza kwamba siku ya uteuzi mgombea aliyetimiza masharti ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kipengele cha 46 cha Katiba ya Zanzibar baada ya kuchaguliwa atarejeshewa dhamana ya fedha aliyotoa mgombea huyo wakati aliporejesha fomu zake.
Akizungumza na wana CCM waliokusanyika katika Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kaskazini “B” hapo Mahonda Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwashukuru na kuwapongeza Wanachama wote waliojitokeza kumdhamini katika mchakato huo.
Balozi Seif alisema ushirikiano waliomuonyesha wadhamini pamoja na wanachama wengine waliojumuika hapo ni ishara ya mwanzo mzuri wa Chama cha Mapinduzi kuelekea katika ushindi mkubwa kwenye uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu wa 2015.
No comments :
Post a Comment