Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, August 18, 2015

Chadema yakomba vigogo UWT, wasomi zaidi Arusha.

  Mwenyekiti wa UWT Monduli, alisema kulikuwa na uvunjaji wa kanuni katika kura ya maoni.

Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe.
Wenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Monduli na Ngorongoro wamejitoa katika chama hicho na kujiunga na Chadema.
Mwenyekiti wa UWT Monduli, Einothi Leringa, alisema kulikuwa na uvunjaji mkubwa wa kanuni chama katika kura ya maoni.
Alisema alikuwa akigombea udiwani wa Viti Maalum Tarafa ya Kisongo, lakini kutokana na chama hicho kushindwa kufuata kanuni za uchaguzi ameamua kwa hiari yake kukihama chama hicho.
Alisema amechukua uamuzi huo licha  ya kwamba alikuwa mpiga debe mkuu wa mbunge wa Viti Maalum aliyemaliza muda wake, Namelok Sokoine, na kumwezesha kupata ushindi mkubwa wa kuwa mgombea ubunge Jimbo la Monduli kupitia CCM.
Katika barua yake ya kukihama chama hicho aliyoiandika Agosti 12, 2015 kwa ofisi ya CCM wilayani humo, Einothi, alisema amekihama chama hicho kwa hiari yake.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ngorongoro, Ruth Mweisari, alisema ndani ya CCM mambo ni yale yale, watu ni wale wale, na matendo ni yale yale.
Alisema ndani ya CCM mtu hawezi kutimiza ndoto yake hivyo ameamua kwa hiari yake kujiondoa katika chama hicho.
Mwenyekiti huyo alirudisha kadi zake za Umoja wa Vijana wa TANU ya mwaka 1967, kadi ya Umoja wa Wanawake wa Tanzania, kati ya Jumuiya ya Wazazi na kadi ya CCM.
 “Nimeamua kwa hiari yangu kuwa na mabadiliko…nilikuwa naipenda sana CCM, lakini imefika wakati naona hakuna mabadiliko, najiunga Chadema kwenda kuchapa kazi,” alisema.
Wengine waliojiunga na Chadema ofisi ya Mkoa wa Arusha jana ni Mhadhiri Mwandamizi wa Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Nelson Mandela, Wakili Dk. Elimani Laltaika na mhitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Ponja Tayai.
Dk. Laltaika kabla ya kujiunga na Chadema alikuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Ngorongoro kupitia tiketi ya CCM na katika kinyang’anyiro cha kura ya maoni alipata kura 10,000.
“Tumefanya kampeni siku 10 na nikapata kura 10,000 hizo ni sawa na kura 1,000 kila siku,” alisema na kuongeza: 
“Lakini kilichojitokeza ni kwamba kura zilipindishwa na waliopiga kura wengine walitoka Kenya.”
Alisema alitumia siku 10 kujinadi katika kampeni za kuwania kuteuliwa ubunge katika jimbo hilo na akafanikiwa kupata kiasi hicho cha kura.
Alisema alijiunga na CCM miaka 11 iliyopita, lakini sasa amevutwa na hotuba ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, aliyozungumzia suala la kuwa taifa lenye ndoto.
“Nimejiunga na Chadema ili hii ndoto ya taifa iwe kutekelezeka…sisi ndio watu tuliokuwa tukisubiriwa na nitaweka alama.
Kwa upande wake, Tayai aliyekuwa akigombea nafasi ya udiwani katika Kata ya Nainokanoka kwa tiketi ya CCM alisema  kura za maoni zilitawaliwa na mizengwe na rushwa na hivyo haki yake ilidhulumiwa.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Njaile, Lazaro Saitoti, ambaye pia awali alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Ngorongoro, alisema ameandika barua ya kujitoa CCM.
“Nimechoshwa na ahadi hewa ambazo zinatolewa na CCM.
“Kuendelea kuwa bado CCM ni sawa mwanachama aliyekufa na kadi…ni bora kabisa kuokota takataka barabarani kuliko kuwa ndani ya CCM,” alisema.
Akiwapokea wanachama hao wapya, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema, Mkoa wa Arusha, Cecilia Ndossi, alisema chama hicho sio chama cha kukaa isipokuwa ni chama cha kufanya kazi.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment