Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, August 31, 2015

Dk. Shein ataka zitafutwe njia mbadala uchumaji karafuu.

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amewataka wataalam wa kilimo kutafuta mbadala wa vifaa vya asili vya kuchumia karafuu ili karafuu za Zanzibar ziendelee kuwa na ubora wake. 
Akizungumza wakati alipotembelea Maonyesho ya Kilimo cha karafuu muda mfupi kabla ya kuzindua mfuko wa kuendeleza zao hilo mjini hapa juzi, Dk. Shein alisema iko haja ya kutafuta mbadala wa vifaa hivyo kama vile pakacha ambazo ndiyo kifaa asili cha kuchumia karafuu zikiwa mtini.
“Hivi sasa watu wengi hawajui hata kusuka pakacha lakini ni ukweli kuwa hata minazi ya kukata makuti ya kutengeneza pakacha imekuwa ikipungua hivyo tunahitaji mbadala wake,” alisema.  Dk. Shein alisema hayo baada ya Ofisa Misitu na Maliasili, Badru Kombo Mwamvura, kueleza kuwa ili karafuu ziweze kuwa katika ubora wake kwa muda mrefu kabla ya kuchambuliwa, matumizi ya pakacha ni jambo muhimu la kuzingatiwa.
Alisema pakacha zinazihifadhi karafuu zikiwa mbichi bila kunyauka kwa muda mrefu na kuwa rahisi kuzichambua kutoka kwenye vikonyo vyake tofauti na ikiwa zimewekwa kwenye vyombo vingine kama viroba au magunia ambako hunyauka haraka na kuwa vigumu kuzichambua.
Katika maonyesho hayo, Dk. Shein alishuhudia hatua mbalimbali za uimarishaji kilimo cha karafuu ikiwamo kazi za kitafiti kama vile aina ya udongo unaofaa katika kuotesha vitalu vya miti hiyo katika sehemu mbalimbali za kisiwa cha Pemba. 
Aidha, aliangalia njia bora za kushughulikia karafuu kuanzia wakati wa kuchuma hadi kuzikausha na kuzipelekea katika vituo vya manunuzi ili kupata daraja za juu na kuongeza thamani ya zao hilo.
Naye Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC),  Mwanahija Almasi Ali, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mfuko wa Kuendeleza Karafuu alisema shirika lake limepata mafanikio makubwa katika kutekeleza majukumu yake hadi kufikia kutambuliwa kimataifa.
“Tumetunukiwa tuzo ya kimataifa iliyoambatana na cheti kutoka taasisi ya kimataifa ya Global Trade Leaders Club ya Hispania kutokana na utendaji mzuri na utoaji wa bidhaa bora na huduma nzuri zinazotolewa na shirika” alisema  Mwanahija. 
Alisema shirika lake linajivunia maendeleo hayo na kutambua mchango mkubwa wa Rais Dk. Shein katika kuhakikisha kuwa zao la karafuu linarejea katika nafasi yake ya kuimarisha uchumi wa Zanzibar na kuendelea kuwa nembo ya visiwa vya Unguja na Pemba.
Alizitaja kazi za Mfuko Maendeleo ya Karafuu kuwa ni pamoja na kutoa mikopo kwa wakulima wa zao hilo, kutoa fidia kwa wanaoanguka mikarafuuni kupitia bima ya ajali na kusaidia upatikanaji wa vifaa vya kukatia miche kwenye vitalu binafsi na vya serikali ili kuongeza idadi ya miche ya mikarafuu.
Kazi nyingine ni kutoa elimu kwa wakulima kuanzia upatikaji, upandaji na huduma za miche ya mikarafuu, kusaidia tafiti na utibabu wa mikarafuu pamoja na kusaidia miradi ya maendeleo ya miundombinu katika mashamba ya maeneo ya zao hilo.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment