Akihutubia kuhusu kujiuzulu kwa Prof Lipumba Makamo huyo wa Rais alieshangazwa kwani Lipumba ndiye muasisi wa UKAWA na pia ndiye alikuwa Mwenyekiti wa wenyeviti wa UKAWA.
maalim Seif pia alisema Profe Lipumba ndiye alimkaribisha Lowassa UKAWA na ndiye alikuwa mtu wa kwanza kumsafisha na kumwagia sifa kem kem.
Maalim seif aliwaambia wanachama hao kwamba UKAWA iko imara kabisa na kwa njia yoyote lazima Edward Lowassa aingie madarakani kwani hana msamiati wa kushindwa na akamuonya Magufuli kwamba IKULU ataisikia tu.
Muda wote Maalim Seif alikuwa akishangiliwa kwa nderemo na umati huo wa wafuasi wa CUF hasa alipokuwa anaitaja UKAWA.
No comments :
Post a Comment