Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, August 29, 2015

Kikwete atahadharisha kauli za uvunjifu wa amani


  • Rais Kikwete alisema hayowakati akizindua Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao jijini Dar es Salaam
By Herieth Makwetta, Mwananchi Digital
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amesema baadhi ya kauli zinazotolewa na Umoja wa Vyama vya Upinzani (Ukawa), zinaashiria uvunjifu wa amani pindi matokeo ya kura yatakapoanishwa baada ya zoezi la upigaji kura Oktoba 25 mwaka huu.
Rais Kikwete alisema baadhi ya kauli hizo zimekuwa zikionyesha wazi viashiria vya uvunjifu wa amani na upotoshaji kwa kundi kubwa la vijana ambao wanapiga kura kwa mara ya kwanza.
Akizungumza wakati akizindua Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao jijini Dar es Salaam Rais Kikwete alisema;
“Wamediriki kusema wazi bila kificho kwamba patakuwa hapatoshi, hizi ni kauli zinazoashiria uvunjifu wa amani. Tunachokisema CCM ushindi kwetu ni lazima na tutashinda kwa kishindo na kwenda nginja nginja mpaka Ikulu.”
Kikwete alisema CCM imejipanga kuhakikisha inapata ushindi katika Uchaguzi Mkuu ujao na kuongeza kuwa ili kufanikisha hilo wamepanga kikosi kazi ambacho kitatembea nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba, mtu kwa mtu ikiwa kwa sasa tayari wameshaanza kufanya kampeni zao kupitia mtandao ya simu za mkononi.
Katika hafla hiyo ya kuzindua kampeni hiyo inayoratibiwa na msanii wa filamu na Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu, Rais  Kikwete aliwataka wanawake kaungalia mazuri yote yaliyofanywa na Serikali ya CCM katika kumuinua mwanamke.

No comments :

Post a Comment