Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, August 31, 2015

CCM Z’bar yaunda ‘timu ya ushindi’

Makamu Mwenyekiti wa CCM , Zanzibar na Rais Dk Ali Mohamed Shein akisalimiana na wajumbe wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar baada ya kumalizika kwa kikao na kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi Kuu ya Chama hicho Kisiwandui jana. Picha na Anthony Siame

By Hassan Ali, Mwananchi
Zanzibar: Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, Zanzibar iliyokutana mchana jana, Kisiwandui imeunda timu ya kampeni za uchaguzi.
Kikao hicho chini ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais Ali Mohamed Shein kiliteua timu ya watu 20 itakayoongozwa na Balozi Seif Ali Iddi akiwa mwenyekiti na katibu wake, Vuai Ali Vuai.
Wengine katika timu hiyo ni Waziri Kiongozi mstaafu,  Shamsi Vuai Nahodha, Haji Mkema Haji, Hamad Yussuf Masauni, Waride Bakari Jabu, Seif Shaaban Mohamed, Najma Murtaza Giga, Dk Maua Abeid Daftari na Profesa Makame Mbarawa.
Wengine ni Omar Yussuf Mzee, Ramadhan Abdalla Shaabani, Mohamed Aboud Mohamed, Khadija Hassan Aboud, Haroun Ali Suleiman, Issa Haji Ussi Gavu, Mahmoud Thabit Kombo, Shaka Hamdu Shaka, Balozi Ali Abeid Karume na mwakilishi ambaye kikao hicho kilishindwa kutaja jina lake akitokea jumuiya ya wanawake  wa CCM.
Vuai ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, alisema kikao hicho pia kililenga kuandaa mikakati mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu na kuhakikisha kinakipata ushindi wa kishindo, kwa wagombea urais wa Muungano na wa Zanzibar, Dk John Magufuli na Dk Shein.


No comments :

Post a Comment