Mgombea Urais wa Chama cha Wakulima Mhe Said Soud Said akiwa na Wanachama wake wakimshindikikiza Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar akiwasili katika viwanja vya Salama Bwawani zilioko Afisi za Tume kuchukua Fomu.
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)Ndg Salum Kassim Ali , akitowa maelezo na kumkaribisha Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Mhe Jecha Salum Jecha kukabidhi fomu hiyo kwa Mgombea katika Afisi za Tume zilioko Ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jecha Salum Jecha akisoma mmoja ya Fomu zinazotakiwa kujaza kwa mgombea kabla ya kumkabidhi kabrasha hilo. Utoaji wa Fomu za Urais zinatolea katika Afisi ya Tume Ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar.
Mgombea Urais akiwa na Wapambe wake waliomshindikiza katika hafla hiyo ya kuchukua Fomu kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia Chama chake cha UPDP,Mhe Mwajuma Ali Khamis akifuatilia makini maelezo yaliokuwa yakisomwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tune ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jecha Salum Jecha akimkabidhi Fomu Mgombea Nafasi ya Urais kupitia Chama cha Wakulima (AFP)Mhe Said Soud Said, hafla hiyo imefanyika katika Afisi za Tume Bwawani Zanzibar.
Mgombea Urais wa Chama cha Wakulima AFP Mhe Said Soud Said akionesha mkoba wake wa fomu za kugombea Urais wa Zanzibar baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)Mhe Jecha Salum Jecha katika Afisi za Tume Bwawani Zanzibar
Wanachama wa Chama cha Wakulima AFP, wakimshangilia Mgombea wao baada ya kuchukua Fomu ya Kuwania Nafasi ya Urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.2015
/ZanziNews.
No comments :
Post a Comment